Habari na Ezekiel Kamanga,Sumbawanga Vijijini.
Taifa
linaweza kuingia katika hatari ya kudidimia kwa uchumi kufuatia watu
wasiokuwa na mapenzi na taifa hili kuziharibu noti za shilingi 500 na
2000 kwa kuondoa mstari(ufito) unaong'aa na unaohalalisha pesa hizo na
kisha kuutumia katika pombe za kienyeji au bia ili kuongeza kileo
wakidai kuwa husaidia kuokoa pesa kwani hulewa kwa muda mfupi.
Mbali
na hivyo mstari huo(ufito) pia huzichanganya na sigara au tumbaku
ambapo hudai hulewa haraka,hivyo kufanya uadimu wa noti hizo katika
maeneo ya Kijiji cha Maleza,Kata ya Kipeta,Wilaya ya Sumbawanga
Vijijini.
Athari
hiyo pia imevikumba vijiji vya Kilangawana na Kamsamba hali ambayo
imefanya kuwepo kwa ugumu wa upatikanaji wa fedha hizo.
Hata
hivyo wananchi kadhaa ambao hawakupenda majina yao
kutajwa,wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuitaka Serikali na
Benki Kuu kuchukua hatua za haraka ili kukomesha vitendo hivyo.
Katika
hali ya kuhalalisha noti hizo zilizoharibiwa wahalifu hao hutumia gundi
kwa kutumia uzi wa mifuko ya mbolea ili ziendelee kutumika na hivyo
kuzalisha noti bandia.
Wakati huohuo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema wanapopokea noti hizo na pia kuwafichua wahalifu hao.
0 comments:
Post a Comment