Na Gabriel Mbwille, Mbeya.
Imedaiwa kushuka kwa uwajibikaji na utendaji kazi wa
watumishi wa idara mbalimbali hapa nchini vikiwemo vyombo vya habari kukosa
maadili kunatokana na mfumo mbovu wa elimu ya hapa nchini.
Hayo yalisemwa na waandishi wa habari mkoani Mbeya wakati wa
mafunzo ya uandishi wa habari kwa njia za mtandao ambayo yameandaliwa na umoja
wa klabu za wa andishi wa nchini (UTPC)
yaliyofanyika katika ukumbi wa hospitali ya mkoa Mbeya.
Walisema kuwa hivi sasa kumekuwa na tabia ya ajira kutolewa
kwa kuangalia kigezo cha elimu pekee pasipo kuangalia ujuzi na uzoefu wa
mfanyakazi kikazi na kimazingira haliinayopelekea kuajiliwa kwa watu waio na
ufahamu wowote wa kile wanachokifanyia kazi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo Saidi Benjamini alisema hivi
sasa ni jambo la kawaida kwa mtu kuajiliwa mara baada ya kumaliza mafunzo
pasipo kupewa elimu ya mazingira ya kazi hali inayopelekea idadi kubwa ya
watumishi wa Serikali kudanga takwimu kwa jamii na taifa.
Naye mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Hawa Mathias
alisema kutokana na teknolojia kukua baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia
takwimu na tafiti kutoa elimu kwa wananchi pasipo kuangalia uhalisia wa eneo
husika na kwamba tabia hiyo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa elimu
inayotolewa ndani ya jamii kutofanikiwa kwa sehemu kubwa kutokana na kutoendana
na uhalisia wa eneo husika.
Naye mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani
Mbeya Christopher Nyenyembe alisema kuwa utafiti kabla ya kuandika habari ni
moja ya taratibu za kazi kwa mwandishi bora na kuwataka waandishi wa habari
kufanya tafiti kwakina ndani ya jamii kabla ya kuiandika habari badala ya
kutumia tafiti zilizopo kwenye mitandao kwa sababu tafiti nyingine zimekuwa
haziendani na uhalisia wa mazingira ya kazi.
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Maggid Mjengwa
alisema tabia ya Serikali kuangalia zaidi vyeti vya elimu ndiyo matokea ya sasa
kwa wanafunzi kuhitimu elimu yao
ya msingi pasipo kujua kusoma wala kuandika.
Aidha tabia ya kuaingiza siasa na maarifa imekuwa ikichangia
kwa sehemu kubwa kukwamisha maendeleo ya elimu hapa nchini ambapo hivi karibuni
tumeona Taifa limeamua kuacha mfumo wa mwanafunzi kuonesha nini amejifunza kwa
kipindi chote na tumeingia kwenye mfumo wa mwanafunzi kukisia majibu.
"Hivi karibuni Tanzania imengia kwenye mfumo wa
usahihishaji wa mitihani ya darasa la saba kwa njia ya mtandao ambapo wanafunzi
watakuwa wakiweka vivuli kwenye majibu sahihi badala ya wanafunzi hao kuonesha
uwezo walionao kutokana na yale waliyofundishwa ambapo hii inahatarisha zaidi
kwa taifa kuwa na wanafunzi wasio na uelewa na elimu kwa sababu ya kuandika
majibu yao kwa njia ya kukisia pia huenda ikawa ni njia kubwa ya wanafunzi
kupewa majibu ya mtihani kuliko hata tatizo la awali
lililojitokeza"alisema Mjengwa
0 comments:
Post a Comment