Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
JESHI
la polisi Mkoani Mbeya linawashilia wanafunzi sita akiwemo Mkuu wa
Chuo cha uuguzi Chimala Francis Mteja kwa tuhuma za kuhamasisha
vurugu zilizopelekea kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya Mbarali
Gulamu Hussen Kiffu kuvunjwa vioo,kutoa upepo wa matairi baada ya
serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi.
Akizungumza
Kamanda wa polisi mkoni mbeya.Athuman Diwani alisema kuwa tukio hilo
lilitokea jana majira ya saa 11 za jioni baada ya mkuu wa wilaya
kuongoza na baadhi ya viongozi wa serikali hususan kamati ya ulinzi na
usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea
kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe.
Aidha
kamanda Diwani amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Mkuu wa
Chuo Francis Mtega () steven Mapunda (19) Isaya Katuwa (23) Lugano
Mwalupasya (22) emmanue bukuku (24) na steven Mapunga ambao wanatarajia
kufanya mtihani wiki ijayo ya kuhitimu mafunzo ya uuguzi.
Aidha
alisema kuwa kutokana na upelezi kukamilika watuhumiwa watano
watafikishwa mahakani leo ambapo mkuu wa chuo atafikishwa mara baada ya
uchunguzi kukamili
Alisema
muda mfupi kwa lengo la kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi
ya wanafunzi walivamia gari la mkuu wa wilaya na kuaza kuvunja vioo
kwa kutumia mawe,na kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.
“Tukio
hilo lilitokea jana na linaonyesha ni mpango uliokuwa umepangwa na
uongozi wa chuo kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania na
lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe ili kitambulike serikali na
kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira
itakayotambulika serikalini”Alisema
“Ni
kitu cha kushangaza sana mkuu wa chuo ni mwalimu huyo huyo,mhasibu,na
kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali kilikuwa ni kitu
cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo na uchunguzi umebaini chuo hicho
kimeanza muda mrefu na tayari kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja
mbalimbali bila ya serikali kutambua kama hakijasajiliwa na
hakitambuliki ’Alisema.
Aidha
diwani ametoa onyo kwa wanafunzi katika vyuo kutojiingiza katika
mikumbo isiyokuwa na tija na hivyo kuchangia kuisabishia hasara serikali
kutokana na uharibifu uliojitokeza katika vurugu hizo na kuongeza kuwa
watuhumiwa wa takaobainika kuhusika katika vurugu hizo watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Diwani
alisewa mpaka sasa wanafunzi wanaoshilikiwa 32 ambapo kati ya hao 5
ndio waliobainika kuhusika na vurugu hizo na wanatarajiwa kufikiswa
mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili ili sheia ichukue
mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine.
Akizungumza
kwa njia ya Simu Mkuu wa Wilaya ya Mbarali . Gulamu Hussen Kiffu
alikiri kutokea kwa vurugu hizo zilizotokana na uamuzi wa serikali
kufunga chuo hicho kutokana na kutokuwa na sifa ya kufundisha na
kudaili wanafunzi wa fani ya uuguzi kwani kilikuwa hakina hati ya
utambulisho wa usajiri serikalini.
Kiffu
alisema kuwa baada ya serikali kutambua tatizo hilo ndipo walipo
kumuhita Mkuu wa Chuo hicho Francis Mteja katika kikao cha kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ambapo aligoma kuhudhuria na kueleza kuwa
yeye anaendelea kufundisha ndipo walipolazimika kufika chuoni hapo jana.
“Serikali
ilikuwa na lengo zuri sana na chuo hicho lakini kutokana na uelewa
mdogo ndio imeweza kutokea hali hiyo kwani serikali haiwezi kuvumilia
vyuo kuendeshwa kienyeji wakati huo watu watakaohitimu hapo watapata
ajira katika vituo vya afya ,hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa
watanzania wasiokuwa na hatia kiafya.”Alisema.
Aidha
baadhi ya wanachi Mkoani mbeya wamelaani vikali tabia hiyo na kuitaka
serikali kuchua hatua za makusudi kwani kufanya hivyo ni uvunjifuni ya
nchi yetu na taifa kwa ujumla kwani kiongozi wa serikali anapaswa
kuheshimwa kwani ndio kiungo kikuu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Aidha
uchunguzi uliofanywa na mwananchji umeabaini kuna baadhi ya wananchuo
walikuwa wametoka katika mazoezi ya vitendo katika vituo mbalimvali
vya afya na wanatarajia kufanya mitihani ya kuhitimu jumatatu na hivyo
kujikuta wakiingia hasara kutokana na chuo hicho kufungwa.
0 comments:
Post a Comment