Iliwahi kuripotiwa
kuwa Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu,
aliipinga Tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel
Nchimbi kuchunguza mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi.Moja ya sababu
alizotoa Lissu ni Tume hiyo kuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu
Stephen Ihema,ambaye alimtuhumu kuwa na rekodi ya utendaji kazi yenye
walakini.
Katika pitapita yangu mtandaoni, nimekutana na habari inayomhusu Jaji Mstaafu Ihema,
ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu vya
Uwindaji wa Kitalii, na sasa kamati hiyo imevunjwa kutokana na
kulalamikiwa mno kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wajumbe.
Binafsi nimeguswa sana na habari hii hasa kwa vile inahusu tuhuma za
rushwa kwa kamati iliyokuwa inamjumuisha Jaji Mstaafu Ihema.Sasa
tukiamini kuwa Jaji Ihema ameshindwa jukumu la ujumbe tu kwenye tume
hiyo ya ushauri,kwanini tumwamini kwenye uenyekiti wa kamati ya
uchunguzi wa kifo cha marehemu Mwangosi?
Wakati ninawapongeza wanahabari waliojitokeza jana kuifahamisha bayana
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wanalaani vikali mauaji ya
mwanahabari mwenzao yaliyofanywa na jeshi la polisi,ningependa kushauri
kuwepo upinzani zaidi dhidi ya Tume hii ambayo kuna kila dalili kwamba
itaishia kuwa kiini-macho tu.Awali,hofu yangu kuhusu Tume hiyo
ilielemea zaidi Watanzania wameshashuhudia utitiri wa tume ambazo mara
nyingi ripoti zake zimeishia kufungiwa maandazi na vitafunwa vingine
badala ya kuwekwa hadharani//hatua kuchukuliwa.Wengi wetu tunakumbuka
kuhusu tume ya milipuko ya mabomu huko Mbagala na Gongo la Mboto.Hadi
leo hakuna kilichoelezwa kuhusu ripoti ya tume hiyo...and life goes on.
Je wewe ni mdau wa habari? Unapenda kuona uchunguzi wa kifo cha
marehemu Mwangosi unafanywa independently na watu wasio na harufu ya
utendaji kazi wenye walakini?Basi ungana na wanahabari kupiga kelele
dhidi ya tume hiyo ya kisanii
0 comments:
Post a Comment