*Kamati yacharuka yamtaka alipe fidia.
*Vijana watishia kikao cha ndani.
*Diwani akanusha kumbeba mwenyekiti.
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Motomoto Bwana Kassimu Mwagala,amejikuta katika wakati
mgumu baada ya kuitwa na Kamati ya Shule ya msingi Motomoto alipotakiwa
kutolea maelezo suala la kukata miti saba ya shule hiyo kutokana na
shinikizo la vijana kutaka kuongeza uwanja wa shule pasipo ridhaa ya
kamati hiyo.
Akiongea
kwa masikitiko Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Lydia Mdoe,amesema kitendo
hicho kilichofanywa na mwenyekiti huyo nicha dharau,hivyo kuwafanya
waishi kwa hofu shuleni hapo licha ya dhamana waliyopewa na Serikali ya
kulinda mali za shule na mazingira yetu.
Aidha
Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo Bwana Yusuph Tosha amesema ukataji
wa miti hiyo uliofnya na Mwenyekiti wa kijiji ni kuifanya kamati yake
kuonekana haifanyi kazi na ni kuingilia majukumu.
Hali
hiyo ilizua taflani katika kikao ambapo Bwana Mwagala kwa kujihami
aliandamana na kundi la vijana,ambao walifanya fujo katika mkutano na
baadae Diwani wa Kata ya Ruiwa mheshimiwa Alex Mdimilage aliagiza kuwa
vijana wote waitwe Ofisi ya kata watoe maelezo ni kwani walivamia
mkutano usiowaruhusu.
Hata
hivyo kutokana na kukera na kitendo cha Mwenyekiti wa kamati hiyo
ilimtaka kulipa jumla ya shilingi 210,000 ili iwe onyo kwake,ambapo
ametakiwa kuomba radhi,kamati hiyona kutakiwa kuzilipia kabla ya Oktoba
12 mwaha huu.
0 comments:
Post a Comment