Diwani
wa Kata ya Myunga,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya mheshimiwa Godfrey Siame
kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA)(kushoto),alipokuwa akimuonesha mpiga picha wetu moja
ya kati ya makaburi saba yanayodaiwa kuwa waliozikwa waliuawa kwa imani
za kishirikiana kisha kutolewa viungo vyao kama vile meno,sehemu za siri
na Moyo pembezoni mwa Mto Momba.Hata hivyo zaidi ya watu watatu
wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo hawajakamatwa licha ya
kufahamika.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Diwani
wa Kata ya Myunga,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya Mheshimiwa Godfrey
Siame,amedai kutishiwa kuuawa na wafanyabiashara watatu waliopo Wilaya
Momba na Mbozi mkoani hapa.
Hayo
yamethibitishwa na diwani huyo baada ya awali Majambazi wawili
waliokodiwa kutoka Mkoani Morogoro kuuawa na wananchi wenye hasira
kali,ambapo kabla ya mauti majambazi hao walikiri kwa maandishi na
kuibua siri nzito kuwa wao wametumwa na Mfanyabiashara Benard Simundwe,
Kasambilo Mteka na Yohana Simkonda wote wakazi wa Kijiji cha Myunga.
Aidha
Diwani Siame amesema kuwa wananchi walifanikiwa kukamata silaha mbili
aina ya Short Gun ambazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya mauaji yake,simu
mbili zenye SMS ya kutumiwa pesa kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Hata
hivyo vielelezo vyote hivyo vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Jeshi
la Polisi Mji mdogo wa Tunduma mkoani hapa Bwana Wendo na taarifa
kutolewa kwa Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Mbozi Bwana Dudu,lakini
cha kushangaza zaidi mpaka sasa watuhumiwa hao hawajakamatwa na
kufikishwa mahakamani licha ya kuwepo kwa vielelezo hivyo.
Imedaiwa
kufuatia tuhuma mbalimbali dhidi ya wafanyabiashara hao ambao pia
wamedaiwa kujihusisha na mauaji ya kikatili kijijini hapo,Jeshi la
polisi linawashikilia wananchi 14,ambao wanadaiwa kuibomoa na
kuiteketeza kwa moto nyumba ya Mfanyabiashara Simundwe.
Wananchi
waliokamatwa na kufikishwa mahakama ya Wilaya Mbozi kusomewa shtaka la
kesi ya jinai ya wizi wa kutumia silaha na kupora mali ni Alick Siame,
Hosea Sinsungwe, Amani Siame, Musa Siame, Laurent Simsokwe, Lighton
Sichone, Sadock Simwanza.
Wengine ni Osphat Siame, John Simbeye, Jacob Mwakalibule, Paulo Sichona na katika kesi hiyo watoto wawili waliopo chini ya miaka 18 wamehusishwa katika sakata hilo ambao ni Damas Sinzumwi na Zebius Sinzumwi.
Watuhumiwa
wote wamenyimwa dhamana,ambapo kesi yao imeahirishwa na Hakimu Mushi na
itatajwa tena Septemba 24 mwaka huu na watuhumiwa wote wanatetewa na
Wakili wa kujitegemea mheshimiwa Edgar Bantulaki.
Kwa
upande wake mwendeshwa mashtaka wa Serikali anatarajia kurekebisha
mashtaka baada ya kupata marekebisho kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la
Polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani ambapo jalada limewasilishwa kwake.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida simu mbili zilizokuwa na vielelezo
zimekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu waliouawa kitu ambacho
kimewashangaza watetezi wa haki za binadamu akiwemo Mwenyekiti wa mkoa
wa Mbeya Bwana Said Mwadudu,hali inayotia shaka hali ya utendaji kazi wa
Polisi kituo cha Tunduma na Mbozi kwa kushirikiana na wahalifu.
Diwani
Siame alitoa taarifa za kutishiwa kwake kuuawa,lakini amedai
kusikitishwa na kitendo cha Polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa na
hata Septemba 10 mwaka huu mfanyabishara Benard Simundwe alionekana
mahakamani na baadae kuamuliwa na mmoja wa askari wa polisi alimuondoa
eneo la tukio na mfanyabishara biasharaa huyo kuelekea kituo cha polisi
Mbozi hali iliyowashangaza wananchi kwa polisi kudai hapatikani.
Vituo
vya Polisi vya Tunduma,Mlowo na Mbozi vimedaiwa kuwakumbatia wahalifu
na hivi sasa diwani huyo amekuwa akilindwa na wananchi.
0 comments:
Post a Comment