Na Esther Macha, Mbeya
Licha
ya Mkoa wa Mbeya kuwa na idadi kubwa ya Mbwa bado imeonekana kuwa kuna
tatizo kubwa kwa wafugaji kutokuwa na utamaduni wa kuchanja mbwa zao
kwa madai kuwa grama za dawa za uchanjaji kuwa kubwa.
Akizungumza
na Mwandishi wetu ofisini kwake , Ofisa Mifugo wa Mkoa wa Mbeya
Dkt.Solomon Nong’ona alisema kuwa mbwa waliopo katika Mkoa ni wengi
ukilinganisha na waliochangwa kwa Mkoa mzima.
Dkt.
Nong’ona alisema kuwa Mkoa mzima una mbwa zaidi ya 70,000 lakini kati
ya hao waliochanjwa ni wachache ukilinganisha na idadi iliyopo ya mbwa
katika Mkoa.
“Kati
ya julai 2011 mpaka julai 2012 ni mbwa 7,849 ambao ni sawa na
asilimia 10 tu ya mbwa waliochinjwa hili ni tatizo kubwa hivyo kuna
haja wafugaji wa mbwa wakaelimishwa si kutoa saababu za grama kubwa za
uchanjaji”alisema.
Hata
hivyo alisema Mbeya jiji pekee kwa wiki inakuwa na matukio 20 ya watu
kuumwa na mbwa na kwamba wilaya ambazo zinaongoza ni pamoja na Mbeya
Jiji ambapo watu 223 waliumwa na Mbwa, Mbozi 206,Chunya 64.
Aidha
Ofisa Mifugo huyo alisema kuwa wafugaji wa Mbwa hawako makini na mifugo
yao kwa kuona hakuna umuhimu wa kuchanja mbwa zao ambazo zinaleta
athari kwa jamii.
Akizungumzia
kuhusu grama za uchanjaji alisema kila mbwa anachanjwa kwa sh.5000
lakini badala yake wafugaji wa mbwa wamekuwa wakiona hiyo ni fedha
nyingi na kuacha mifugo hiyo ikiendelea kuteketeza maisha ya wananchi
wakati uwezo wa kuwachanja upo.
“Grama
ambayo mimi naweza kuiona ni kwa mtu ambaye ameumwa na mbwa kwani
Wilaya zingine hakuna hiyo dawa ambapo humlazimu mwananchi kupanda gari
na kuja Mkoani kupata dawa hiyo kwa kutumia fedha ili aweze kufika
hapa,ni jana tu alikuja mwananchi mmoja kutoka Ileje ambaye aliumwa na
mbwa ”alisema.
Aidha alitoa wito kwa wafugaji wa mbwa kufuga mbwa na paka kwa ustaarabu ili zisiweze kuleta athari kwa jamii .
0 comments:
Post a Comment