Na
Ezekiel Kamanga, Chunya.
Wakunga
wa jadi wawili wanaofanya shughuli ya kuwazalisha wanawake wajawazito katika
Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamewaokoa wanawake wengi,licha ya
kukabiliwa na Chnamoto mbalimbali katika
ufanikishaji wa fani hiyo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi.
Mmoja
wa wakungunga anayefahamika kwa jina la Bi.Hilda Said Kawinga(80),amesema mpaka
sasa amewazalisha wajawazito 55 mwaka huu na walipokelewa kwake siku mojakbalya
yakujifungua na hakuna kifo chochote kilichowahi kutokea na kuorodhesha katika Daftari lake na ilimlazimu kufanya hivyo ili
kuisaidia Serikali kupata takwimu endapo zitahitajika,
Amesema
kuma kuwa changamoto aliyonayo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya studio kama
vile mkasi,vyombo vya kuhifadhia maji,kitanda na godoro ambapo amesema kwa
wastani hupokea zawadi ya wajawazito 10 kwa mwezi na hakuna tozo kwa huduma
hiyo mara baada ya kujifungua.
Kwa
upande wake Mkunga mwingine Bi, Agripina Fredrtick Sikanyika (37) maarufu kama Mama Namwinji,amesema imemlazimu kuwaachia nyumba
wagonjwa wanaofika kwa ajili ya kujisubiria kutokana na mfululizo wa wagonjwa
hao wanaofika kwake kupata huduma hiyo huku akiacha nyumba nyingine kwa ajili
ya kujifungulia.
Mkunga
huyo amesema alianza huduma hiyo tangu mwaka 2000 na mwaka 2011 alizalisha
wajawazito 114 na mwaka huu wajawazito 187 na kwamba kati ya hao watoto wawili
walizaliwa wakiwa na ulemavu wa aina yake.
Mnamo
Septemba 15 mwaka huu mwanamke mmoja alijifungua mtoto mwenye sikio moja, mguu
mmoja, mdomo na pua vikiwa vimeungana ma mtoto huyo alifariki muda mfupi baada
ya kujifungua.
Aidha
Septemba 16 mwaka huu pia alizaliwa mtoto aliyekuwa na kichwa mithili ya
ng'ombe na kiwiliwili cha binadamu.
Mbali
na matukio hayo mawili ya aina yake,mkunga amesema kuwa yeye hatozi tozo yoyote
licha ya kazi ngumu ambayo amekuwa akiifanya usiku na mchana huku ukiwepo uhaba
wa kitanda cha kujifungulia wajawazito kwani huwalaza chini na kukabiliwa na
magonjwa hasa kipindi cha masika.
Aidha
Bi Agripina amesema kuwa hufuata taratibi zote za kuwapokea wajawazito hao kwa
kuzikagua kadi za kliniki na kuzijaza
pindi wakijifungua.
Mbali
na hilo mkunga huyo pia hupokea wajawazito ambao
wanatakiwa kufanyiwa oparesheni/upasuaji na kwake hujifungua salama bila
upasuaji wowote na kubainisha kuwa mmoja wa wajawazito alifanyiwa upasuaji kama mara mbili hospitalini lakini alipopelekwa kwake
alijifungua watoto wawili salama katika nyakati tofauti.
Hata
hivyo Bi Agripina ametoa wito kwa serikali kuwasaidia wakunga kutokana na
kufanya kazi hizo ngumu ambazo zingefanywa hospitalini na pia amesikitishwa na
kitendo cha Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni kumtoza shilingi laki mbili kwa
kile alichodai kuwa ni kifo cha mama mjamzito na stakabadhi ya malipo kutopewa.
0 comments:
Post a Comment