Habari na Ezekiel,Kamanga.
Mwanamke
mmoja Vi Matrida Charles(42) Mkazi wa Kitongoji cha Motomoto B,Kijiji
cha Motomoto,Kata ya Ruiwa,Welaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,anaishi na
wanaume wawili kwa wakati mmoja kwa takribani siku nne mpaka hivi sasa.
Tukio
hilo la aina yake lililofanywa na mwanamke huyo baada ya kutelekezwa na
mumewe wa awali Bwana George Mwasomola anayetoka Kijiji cha
Mahango,ambaye ameishi naye kwa mika 25 kabla ya kumtelekeza miaka saba
iliyopita naye kukimbilia Mkoani Morogoro na kurejea Septemba 8 mwaka
huu.
Baada
ya kurejea alimkuta mkewe Matrida akiishi na mwanamke mwingine aitwaye
Idd Msongole(50),miaka saba iliyopita katika nyumba ambayo mwanamke huyo
alijengewa na mwanae ambaye baba yake alifariki kabla ya kuolewa na
mwanamme wake wa sasa anayeishi naye.
Septemba
9 mwaka huu Bwana Mwasomola alimwita mkewe huyo wa zamani nyumbani kwao
Kijiji cha Mahango,ndipo mwanamke huyo akamjibu kuwa aje kijijini kwao
Motomoto na kumtaka mumewe wa saa Bwana Msongole aondoke hapo nyumbani
na alitakiwa kuishi kwa Balozi wa Shina Bwana Mussa Haonga,huku kila
mmoja akipata huduma ya chakula,maji ya kuoga na kila mmoja kutembelewa
kwa nyakati tofauti.
Baada
ya kuona vitimbi hivyo viongozi wa Kitongoji cha Motomoto B ukiongozwa
na Mwenyekiti wake Bwana Andrea Mwambije,aliamua kutoa taarifa kwa
Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Kassim Mwagala ambaye naye alimtaarifu Afisa
Mtendaji wa Kijiji Hussein Mwantanji na baadae Bi Matrida kuulizwa kuwa
yupi ni mume wake halali ambapo alijibu kuwa ni Bwana Idd
Msongole,ingawa ndiye aliyetolewa nyumbani hapo nakwenda kuishi kwa
balozi akimwacha bwana Mwasomola akijivinjari na kuzua gumzo kijijini.
Hata
hivyo uongozi wa kijiji umekuwa na wakati mgumu endapo mmoja kati ya
wanaume hao atakapo taharuki hivyo umetoa taarifa katika Ofisi za Kata
na Kituo cha Jeshi la Polisi Igurusi ili kuchukua tahadhari.
Aidha
katika uchunguzi umebaini kuwa Bwana Idd Msongole ambaye anaishi kwa
Balozi kwa sasa yupo tayari kusubiri hata mwezi mmoja ili Bi Matrida
amalizane na Bwana Mwasomola kuweka saini katika ofisi ya kijiji
kuhakikisha usalama wa wanaume hao,licha ya mwanamke huyo kukiri wazi
kuwa kwa sasa anependa kuishi na mumewe wa sasa Msongole kwa kuwa mume
wake wazamani Bwana Mwasomola alimtelekeza miaka saba iliyopita.
Habari
za ndani zinadai kuwa katika sakata hilo uongozi ulimtoza adhabu ya
shilingi 100,000 mwanamke huyo,ambapo alilipa shilingi 90,000 na mumewe
wa zamani alitozwa shilingi 50,000 na kutakiwa aondoke mara moja.
Wakati
hayo yakijiri Bwana Msongole kila asubuhi alikuwa akifika nyumbani kwa
mwanamke huyo akitokea kwa Balozi na kuichukua mifugo kwenda nayo
machungoni na kurejea majira ya jioni na baadae kuelekea kulala kwa
balozi huku Bwana Mwasomola alikuwa akielekea Mahango kwa ajili ya
biashara.
****Hatima ya kitendawili hiki kitateguliwa na Matrida mwenyewe endelea kufuatilia mtandao huu******.
0 comments:
Post a Comment