*Ni katika shamba la Kapunga Rice Project.
*Wazazi wacharuka na kuanza kujenga shule mpya mahali alipobomoa mwekezaji.
*Zaidi ya shilingi milioni 2.5 zachangwa papo hapo.
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Wanafunzi
23 wa Shule ya Msingi Kapunga,Kijiji cha Mapogolo,Wilaya ya Mbarali
Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya kula mikate inayosadikiwa kuwa
na sumu mnamo mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Ramadhani Nyoni na
mzazi mmoja wapo wa watoto waliokumbwa na janga hilo la kusikitisha na
kuhatarisha uhai.
Mzazi
huyo ambaye hakupenda jina lake kutaja amesema yeye ilimlazimu kununua
lita 20 za maziwa,kisha kuwanywesha watoto hao na kuokoa maisha yao
ambapo hali zao zimetajwa kuendelea vema.
Wakazi
wa kijiji hicho wakionekana kukerwa na kitendo hicho iliwalazimu
kuitisha mkutano wa hadhara na kuazimia kujenga shule mpya ili kuwaondoa
watoto katika shule iliyopo katika shamba la mwekezaji.
Mbali
ya wananchi kukerwa na vitendo vya kikatili vya mwekezaji huyo,pia
Walimu wamefurahia uamuzi wa wanakijiji kuamua kujenga shule mpya katika
himaya ya kijiji ili kuondoa adha ya kutembea umbali wa kilometa 52
kwenda na kurudi kutoka Chimala,ambako ndipo walipopanga kutokana na
uhaba wa nyumba kijijini hapo na zilizopo shambani kwa mwekezaji walimu
hao hufukuzwa mara kwa mara.
Aidha
wazazi hao waliachanga jumla ya shilingi 2,500,000 kwa ajili ya kuanza
ujenzi,ambapo Afisa Elimu kitengo cha Ujenzi amesema atawakabidhi ramani
ya shule,uongozi wa kijiji,ili kuondoa adha ya wakazi zaidi ya 12,000
wanaoishi eneo hilo ambapo shughuli za maendeleo zimedumazwa na
mwekezaji huyo ikiwemo kuhodhi miundombinu kama barabara,umeme na maji.
Licha
ya miundo mbinu yote kupita kijijini hapo lakini wananchi hawanufaiki
nayo bali kuambulia kipigo na kufunguliwa kesi mahakamani pasipo sababu
maalumu.
Hata
hivyo wananchi hao wamesema hawakuona sababu yoyote ya msingi kuweza
kutoa taarifa katika Jeshi la polisi,kutokana na mwekezaji kujaza mafuta
magari pindi magari ya jeshi hilo yanapoenda kijijini hapo.
Wananchi
hao walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa baadhi ya mifugo ya wananchi
imekuwa ikiuawa mara kwa mara na mwekezaji huyo,lakini hakuna hatua
zozote ambazo zimekuwa zikichukuliwa likiwemo tukio la wananchi kugongwa
na gari la mwekezaji ambapo alimfukuza na kisha kumgonga mwananchi
huyo,ambaye kwa sasa amepata ulemavu na mwekezaji kutochukuliwa hatua
zozote tangu mwezi Julai mwaka jana.
Pia
mwekezaji huyo mapema mwezi Januari mwaka huu alichoma mpunga wa
wakulima kwa kunyunyizia dawa kupitia ndege ya umwagiliaji na
kusababisha zaidi ya wananchi 150 kuathiriwa na sumu hiyo ya mimea na
kuwasababishia hasara kubwa,ambapo njaa inatazamiwa kuwakabili wananchi
hao.
0 comments:
Post a Comment