Habari na Gabriel Mbwille,Mbozi.
Wakulima
wa zao la kahawa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,wamesema biashara ya
uuzaji wa kahawa Mbichi imekuwa ikiendelea kufanyika licha ya Serikali
ya mkoa kupipiga marufuku biashara hiyo kutokana na baadhi ya watendaji
wa Serikali kujihusisha na ununuzi wa kahawa hiyo.
Wakiongea
na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wa kulima wa zao hilo katika kata
ya Mlangali wilayani humo wamesema mtandao wa biashara ya kahawa mbichi
(CHERY) umekuwa ukifanywa na watendaji wa Serikali kupitia mawakala
ndiyo maana wameshindwa kuwadhibiti.
Aidha
mmoja wa wakulima hao Batholomeo Mwayela wamesema mkulima anayeuza
kahawa mbichi hupata hasara zaidi ya mara tatu ukilinganisha na bei ya
kahawa inayokobolewa.
Kwa
upande wake afisa kilimo wa kijiji cha Lukululu kata ya Mlangali
Bi.Miriam Philipo amewataka wakulima kuwa na tabia ya kuweka akiba ya
fedha ili ziweze kuwasaidia katika msimu wa mavuno.
Wakati huohuo amesema wakulima waekuwa wakipata hasara kubwa kupitia biashara hiyo na Serikali
imeombwa kusimamia soko la zao la kahawa ili kuwezesha kuwepo kwa bei
itakayomnufaisha mkulima kutokana na kutokuwepo kwa bei maalumu katika
msimu wa mavuno wa zao hilo.
0 comments:
Post a Comment