Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwimbaji
wa nyimbo za Injli mkoani Mbeya Bwana Yona Mwaisango amekanusha
kufumaniwa akiwa na mke wa mtu katika mtaa wa Ilolo Kati,Jijini Mbeya
Julai 2 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku.
Mwimbaji
huyo amesema hiyo ilikuwa ni mbinu tu zilizopangwa ili kumchafua yeye
kwani alifika nyumbani hapo(inapodaiwa alifumaniwa) kwa lengo la
kumsaidia hudumua ya chakula na mpango wa kuwaelimisha ili waweze
kukopa katika Shirika la mikopo la PRIDE .
Ameongeza
kuwa alidaiwa pesa za ugoni shilingi laki tano na kuziahidi kulipa
Julai 3 mwaka huu ambapo alitoa jumla ya shilingi 250,000 na kuahidi
kiasi kilichobaki atakilipa Julai 7 mwaka huu.
Mwimbaji
huyo amekiri kusaini barua ya kulipa faini hiyo na kwamba alifanya
hivyo ili kuepuka kudhurika kutokana na kutishiwa usalama wake kutoka
kwa wananchi wenye hasira kali na kwamba kwa sasa hayupo tayari kuzilipa
pesa hizo kwani hakutenda kitendo hicho cha ugoni na cha aibu.
Aidha
kikao hicho kilifanyika katika nyumbani hiyo(inayodaiwa alifumaniwa
humo) kilichochukua muda wa masaa mawili kabla ya kuruhusiwa kutoka.
Hata
hivyo,wimbi la watumishi wakubwa na kashfa ya ugoni na ubakaji zimezidi
kuwaandama waimbaji mkoani hapa ,ambapo hivi karibuni Uncle Machibula
alidaiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Pili na kushikiliwa kwa siku
kadhaa na kisha kuachiwa huru na Jeshi la polisi mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment