Chifu Merere II wa kabila la wasangu.
******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chifu
Merere II (70) wa kabila la wasangu,amenusurika kuzikwa akiwa hai baada
ya kutokea tafrani katika msiba wa kijana aliyefahamika kwa jina moja
la Frank,katika Kijiji cha Ijumbi,Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani
Mbeya.
Tukio
hilo limefuatia baada ya chifu huyo akishirikiana na ndugu kukubali
kwenda kupiga ramli ya ugonjwa wa kijana huyo baada ya kifo kwa Mganga
wa kienyeji aishie Wilaya ya Mbozi,ambaye jina lake hakutajwa na mganga
huyo kuagiza kuchinjwa ng'ombe mmoja na kupikwa pombe katika pipa lenye
ujazo wa debe 12.
Kufuatia
agizo hilo marehemu aliuza sehemu ya uwanja aliokuwa anaumiliki kwa
zaidi ya shilingi 450,000 na Chifu Merere II kukabidhiwa pesa hizo kwa
ajili ya tambiko.
Aidha
baada ya makabidhiano hayo ng'ombe alichinjwa,pombe kupikwa na kuitwa
baadhi ya wanandugu mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu na kwamba baada
ya tambiko marehemu atapona.Mganga huyo alidai waliomroga marehemu huyo
ni ndugu wa karibu na majirani licha ya kutoweka wazi majina yao.
Sakata
la Chifu Merere II kutaka kuzikwa akiwa hai limekuja baada ya marehemu
Frank kufariki Julai 10 mwaka huu na vijana wa kijiji cha Ijumbi kutaka
maelezo kwanini marehemu amefariki kutokana na sadaka kutolewa huku
marehemu akiuza kila kitu alichokuwa nacho.
Aidha
haikuishia hapo vijana hao waligoma kuchimba kaburi na kumtaka Chifu
huyo atoe maelezo ya kwanini marehemu amefariki lasivyo arudishe pesa
vinginevyo atazikwa akiwa hai ili iwefundisho.
Naye,Afisa
Mtendaji wa Kata Bwana Jordan Masweve,alipopata taarifa hizo alienda
nyumbani kwa Chifu na kukuta vijana wamemzonga wakimdai pesa
zilizotumika katika tambiko.
Hata
hivyo Chifu Merere II alikuwa hana la kujibu,ndipo Afisa mtendaji huyo
alimchukua na kwenda kumfungia mahabusu na yeye kwenda msibani na
kuitisha mkutano wa hadhara,ambapo aliwaomba wananchi wakachimbe kaburi
huku yeye akiahidi kumfuatilia Chifu huyo ili arejeshe pesa hizo.
Pamoja
na vijana hao kukubali kuzika majira ya saa 8 mchana,hali ilizidi kuwa
tete ndipo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman alituma askari
kijijini hapo kwa ajili ya kuimarisha amani na kumwokoa Chifu huyo baada
ya mazungumzo marefu na baadhi ya pesa shilingi 350,000 kurejeshewa
aliyenunua uwanja.
Wakati
kiasi kilichobaki Diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Alex Mdimilage amesema
watafanya utaratibu wa kuzirudisha katika familia ya ndugu wa
marehemu,na chifu Merere II kuachiwa majira ya saa 12 jioni na amani
kurejea kijijini hapo.
Siku chache zilizopita mwanamke mmoja wa Kijiji cha Malamba,Kata hiyo Bi Rozina Mwadala(60),aliyezikwa akiwa hai Juni 2 mwaka huu baada ya kutuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina baada
ya Mganga wa kienyeji huyo huyo kutoka Wilaya ya Mbozi kupiga ramli
kwa madai kuwa marehemu aliyezikwa hai ndiye aliyesababisha kifo cha
mkazi mwingine wa kijiji hicho marehemu Frank Lingo(25),aliyefariki
Juni Mosi mwaka huu kwa maumivu kwenye sikio na jicho.
0 comments:
Post a Comment