Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mahakama
ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Mbeya,umemwachia huru aliyekuwa Hakimu
mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mbeya Amani Mwihomeke(30),aliyekuwa
anakabiliwa na tuhuma za rushwa.
Hakimu
huyo anakabiliwa na makosa mawili kinyume cha sheria kifungu cha 15 cha
kanuni ya adhabu kifungu kidogo(i) cha 11/2007 ambapo alidaiwa
kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 150,000 mnamo Mei 29 mwaka huu.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali kutoka kikosi cha kupambana na kuzuia rushwa
nchini TAKUKURU,Kanda ya Mbeya Bwana Nimrod Mafwele akisaidiwa na Sarah
Martin walidai Mahakamani kuwa Amani Mwihomeke alishawishi na kupokea
rushwa hiyo katika Bar ya Bonanza iliyoko barabara ya Benki Kuu Jijini Mbeya.
Hakimu
mfawidhi wa wilaya ya hiyo a Seif M. Kulita amesema mtuhumiwa anaachiwa
huru kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo
hivyo mahakama kuchukua uamuzi huo wa hukumu ambayo ilichukua masaa
matatu kusomwa katika mahakama hiyo.
Hakimu Mwihomeke alikuwa anatetewa wakili wa kujitegemea Mika Thadayo Mbise.
0 comments:
Post a Comment