Pages


Home » » POLISI YAMNASA MTU MMOJA RAIA WA KENYA KWA KUHUSIKA NA SHAMBULIO DHIDI YA DKT. ULIMBOKA.

POLISI YAMNASA MTU MMOJA RAIA WA KENYA KWA KUHUSIKA NA SHAMBULIO DHIDI YA DKT. ULIMBOKA.

Kamanga na Matukio | 05:32 | 0 comments



Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova.
Na.MO BLOG TEAM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja raia wa Kenya kwa tuhuma za kuteka nyara na shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Dkt. Stephen Ulimboka lilifanyika tarehe 26 Juni 2012.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum Suleiman Kova amesema mtu huyo aitwaye Joshua Gitu Mhindi mwenye umri wa miaka 31, ana kitambulisho cha utaifa Na.29166938 kilichotolewa Nyeri na hati ya kusafiria ya dharura Na.0123431 iliyotolewa Namanga Kenya.

Kamanda Kova amesema katika mahojiano na polisi mtu huyo alieza kwamba yeye ni mwanachama wa kikundi cha kihalifu kinachojulikana kama GUN STAR chenye makao yake eneo la RUIRU wilaya ya Thika nchini Kenya na kudai kuwa kinaongozwa na mtu mwenye jina la utani SILENCE akisaidiwa na PAST, ambao wamekuwa wakifanya matukio mengi ya kihalifu nchini Kenya.

Mtu huyo alipohojiwa zaidi alisema alikuja Tanzania na wenzake 12 kwa lengo la kumdhuru Dkt. Stephen Ulimboka baaada ya kukodiwa na mtu ambaye hakumtaja jina, ambaye anaamini kuwa ni mtumishi wa serikali.

Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wengine waliohusika.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger