Mh. Rais Kikwete akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi na upimaji wa maji katika Kijiji cha Swaya,Wilaya ya Mbeya vijijini Julai 22 mwaka huu.
*********
Na Bosco Nyambege Mbeya
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itamchukulia hatua kali za
kisheria mwananchi yeyote atakayebainika kuharibu vyanzo vya maji
nchini.
Onyo
hilo limetolewa hivi karibuni na Rais Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete,alipokuwa akizindua mradi wa maji safi na upimaji wa maji katika
Kijiji cha Swaya,Wilaya ya Mbeya vijijini Julai 22 mwaka huu.
Amesema
uharibifu wa vyanzo vya maji hupelekea kukosekana kwa maji na hivyo
kusababisha majanga mbalimbali kwa binadamu kama vile ukame,magonjwa
pamoja na vifo.
Aidha
amesema ili kuthibiti tatizo hilo la uharibifu wa miundombinu ya maji
ni vema kila mtu akahusika kulinda vyanzo vya maji vinavyomzunguka,
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka husika waharibifu wa vyanzo
vya maji wanapobainika.
Amebainisha
kuwa serikali itahakikisha inatatua tatizo la uhaba wa maji hapa nchini
ili kumwezesha mwananchi wa kipato cha chini kupata maji safi na salama
kwa wakati muafaka.
Mbali
la hilo Rais Kikwete amewasihi wananchi kulipa bili za maji kwa wakati
muafaka ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi na
wakati.
Mradi
huo wa maji umegharimu kiasi cha shilingi 79.5 bilioni mpaka
ulipokamilika na unatarajia kuhudumia watu zaidi ya laki tatu mkoani
mbeya kwa muda wa miaka mitano ijayo.
Mradi
huo umejengwa kwa udhamini kutoka Ujerumani,umoja wa ulaya-EU kwa
Ushirikiano na serikali ya Tanzania mpaka kukamilika kwake.
0 comments:
Post a Comment