Jinsi
alivyokuwa akiondoka mkutanoni Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyovyo,Kata ya
Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Bwana Rashid Likuta mara baada ya
kuvuliwa madarakani kwa kile kilichodaiwa kuwa anajihusisha na ufujaji
wa pesa za kijiji wa zaidi ya shilingi laki nne na kutosoma taarifa za
mapato na matumizi.
Baadhi ya Wajumbe walioteuliwa kuchunguza ubadhilifu wa pesa za Kijiji cha Iyovyo,wakikamilisha taarifa kabla ya kuisoma.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakisikiliza kwa umakini mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyovyo,Bwana Rashid Likuta.akijitetea kuhusiana na tuhuma zinazomkabili..
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakisikiliza kwa umakini mkutano huo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Iyovyo Bwana Njobeni,aliyepewa madaraka ya
kukaimu nafasi ya Uafisa Mtendaji wa kijiji mara baada ya Serikali ya
kijiji kutenguliwa madarakani kutokana na ufujaji wa fedha za kijiji..
Diwani
wa Kata ya Totowe mheshimiwa Godian Wangala,akiwasihi wananchi
kuendelea kuchangia maendeleo licha ya Halmashauri ya Kijiji kuondolewa
madarakani kutokana na ubadhilifu wa fedha za kijiji.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchunguzi Bwana Michael Mwamlima,akitoa taarifa za kubaini
ubadhilifu huo uliofanywa na uongozi wa kijiji katika mkutano wa kijiji.
Meza na viti vikiwa wazi baada ya viongozi wa kijiji kuvuliwa madarakani(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya).
0 comments:
Post a Comment