Mwanafunzi
wa darasa la 5 akigalagala chini ya sakafu kutokana na mwalimu
kutokuwepo darasani ni katika Shule ya Msingi Iyovyo,Kata ya Totowe
Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Mandhari ya moja ya Chumba cha darasa katika Shule ya Iyovyo.
Wazazi
wa Kijiji cha Iyovyo wakiwa katika malumbano juu ya suala la michango
kufunjwa na Uongozi wa kijiji hivho. Pichani ni chumba cha darasa kikiwa
kimejaa vumbi na baadhi ya wanafunzi kukaa chini.
Katika
kuinua soka kwa watoto walio na umri mdogo,suala la Chandimu huhusika
zaidi kutokana na kutengenezwa pasipo gharama yoyote. Tazama pichani
wanafunzi wameweka mpira juu ya dawati,huku mwalimu akiendelea
kufundisha.
Utumikishwaji
wa wanafunzi katika kazi ngumu kama ubebaji tofari,kuchota maji,kuzagaa
kuni nk, bado ni tete kufuatia wanafunzi wa wilayani Chunya
kutumikishwa katika kazi hizo.
Mwanafunzi akiwa ametoka mtoni kuteka maji ya mwalimu.
Hii
ni moja kati ya adhabu ambayo kwa wanafunzi imekuwa sugu kutokana na
baadhi ya walimu wasiokuwa na utu kuwaadhibu pasipo kujali maumivu
wayapatayo wanafunzi.(Picha na Ezekiel Kamanga, Chunya)
0 comments:
Post a Comment