Pages


Home » » BREAKING NEWSSS:- MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI AFUMANIWA NA AKUBALI KULIPA FIDIA YA SHILINGI 500,000/=.

BREAKING NEWSSS:- MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI AFUMANIWA NA AKUBALI KULIPA FIDIA YA SHILINGI 500,000/=.

Kamanga na Matukio | 05:28 | 0 comments
Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Mkoani Mbeya(jina tunalihifadhi),ambaye pia ni mwalimu wa kwaya moja jijini Mbeya, amefumaniwa katika Mtaa wa Ilolo Kati akiwa na mke wa mtu majira ya saa 3 usiku.

Mwimbaji huyo ambaye pia hujihusisha na huduma kwa watoto yatima,amejikuta akinaswa na mume wa mwanamke huyo aliyekuwa naye na kuokolewa na wasamalia wema,ambapo mwimbaji huyo baada ya majadiliano ya masaa matatu alikubali kulipa fidia ya ugoni ya shilingi 500,000.

Aidha mwimbaji huyo amekiri kutenda kosa hilo na kuahidi leo kulipa shilingi 250,000 na kiasi kilichobaki akidai atamalizia Julai 8 mwaka huu.

Ameongeza kwa kuomba kuhifadhiwa kwa lengo la siri kutovuja na kudai kuwa atakuwa mwaminifu katika ulipaji wa deni na kuondoka baada ya kuacha maandishi na kuweka sahihi mbele ya mwenyekiti aliyejihudhuru hivi karibuni wa mtaa huo wa Ilolo Kati..


*****Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao huu******
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger