Sehemu ya mabati 57 yaliyotolewa na Familia ya Mligula iliyokuwa ikigombea mali za marehemu Eva Emmanual Mligula na Emmanuel Mwaigaga na kutoa vitisho kwa njia ya mtandao kwa Bwana Allan Mwaigaga,ambaye aliitaka familia hiyo kuchangia maendeleo ya Shule tatu za Msingi ya Itewe,Pankumbi na Mwashoma.
Viongozi wa kikabila(Machifu) na wanafamilia wa pande zote mbili za marehemu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza tofauti zao.(Picha na Ezekiel Kamanga)
*******
Habari na Ezekiel
Kamanga,Mbeya.
Ugomvi wa kugombea
mali za marehemu uliokuwa unahusisha familia mbili za marehemu Eva Emmanuel
Mligula(38) na Emmanuel Mwaigaga aliyefariki miaka nane iliyopita waliokuwa
wakiishi Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya umesuluhishwa baada ya
familia hizo kukutanishwa na uongozi wa kimila na Serikali.
Awali ugomvi ulianza
Julai 13 mwaka huu katika mazishi ya Mjane Eva,kufuatia Baba na kaka wa
marehemu huyo kuwazuia ukoo wa Mwaigaga(kiumeni) kutokuwepo katika msiba na
kutohudhuria mazishi kwa kile kilichodaiwa kuwa ukoo unaweza kuuza nyumba ya marehemu.
Mvutano huo ulielekea
ukoo wa marehemu kubeba kila kitu kilichokuwemo ndani zikiwemo samani kwa
kutumia gari yenye nambari T 788 BLK aina ya Fuso na T 314 AVA aina ya Center
na kusababisha Bwana Allan Mwaigaga(Mwaji Group) kutoka ukoo unaotuhumiwa kutoa
taarifa Kituo cha Polisi cha Uyole.
Mkuu wa kituo hicho cha polisi Lazaro Kiyeyeu alifika
eneo la tukio na kushuhudia vyombo vikibebwa na ukoo wa Mligula naye kwa
kushirikiana na Mwenyekiti wa mtaa Bwana
Michael Mwamahondya kuchukua jukumu la kumtaarifu Diwani wa kata ya Uyole Bwana
Ngambi Ngela ambaye aliwasihi wananchi waliokuwepo msibani hapo kurudi makwao
na hivyo na kila familia ya marehemu kwenda kulilia msiba nyumbani kwao na
nyumba hiyo ya marehemu kufungwa na yeye kukabidhiwa funguo kukabidhiwa Bwana
Mwaigaga.
Aidha .baada ya
funguo hizo kukabidhiwa hali ikawa tofauti kutokana na ukoo wa Mligula
kuporomosha matusi na vitisho kwa Bwana Mwaigaga,ambaye alitoa taarifa Polisi
na kufunguliwa kesi mbili dhidi ya ukoo huo,ambapo kesi ya kwanza yenye nambari
MB/IR/57/67/2012 ya kutishia kuua kupitia
njia ya mtandao na kesi ya pili ya Jinai 551/2012 ya kutoa kashifa mbele ya
umma na kupora mali za marehemu.
Mnamo Julai 19,mwaka
huu Katibu wa mila wa kabila la Kisafwa Chifu Mwalwego alipokea ombi la msamaha
kutoka kwa familia ya Mligula kuomba wapatanishwe na ukoo wa Mwaigaga,baada ya
kugundua wamefanya makosa ya kuchukua mali za marehemu badala ya kuziacha
katika nyumba hiyo ambapo marehemu wameacha watoto watatu wawili wa kiume na
mmoja wa kike ambao walipaswa kuacha mali hizo.
Baada ya kupokea ombi hilo Chifu huyo aliwasiliana
na Bwana Mwaigaga ambaye alikubali kusamehe na kutaka akutanishwe na ukoo huo
Julai 21 mwaka huu majira ya saa nne katika eneo la nyumba ya marehemu iliyopo
mtaa wa Utukuyu na kwamba yeye hataki kulipwa fidia yoyote licha ya
kudharirishwa lakini ameutaka ukoo huo uchangie maendeleo katika shule tatu za
msingi zinazozunguka eneo hilo ambazo ni Shule ya Msingi Itewe ipewe mabati 19
ya gauge 30 na shilingi 100,000 kwa Chifu wa mtaa huo.
Ameongeza kuwa Shule
ya Msingi Pankumbi ipewe mabati 19 na shilingi 100,000 kwa chifu wa eneo hilo
na Shule ya msingi Mwashoma ipewe mabati 19 na shilingi 100,000 na Chifu Mwanshinga apewe
shilingi 200,000 kama msuluhishi wa mgogoro huo.
Hata hivyo Julai 21
mwaka huu ukoo wa Mligula,ulilipa shilingi 500,000 na mabati 57 mbele ya
uongozi wa Machifu na uongozi wa Kata ya Uyole baada ya kukutanishwa na ukoo wa
Mwaigaga.
Kwa upande wake Bwana
Allan Mwaigaga alisema hana kinyongo na kuahidi kufuta kesi mahakamani lakini
pande zote mbili za familia zishirikiane kuwalea watoto hao walioachwa na
marehemu,pia mali zituzwe na nyumba ipangishwe ili pesa zitumike kwa ajili ya
kuwasomesha watoto kwani kwa kufanya hivyo iwe fundisho kwa watu wote wenye
tabia za kuhodhi mali za marehemu na kuacha watoto wakihangaika.
0 comments:
Post a Comment