Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Afisa
mtendaji wa Kijiji cha Idimi,Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya
Bwana Amon Myola,ameingia matatani kwa tuhuma za kufuja pesa za michango
shilingi 190,000 kati ya shilingi 746,000 pamoja na mifuko 16 kati ya
30 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mchungaji Luckson
Mwanjale.
Hayo
yamebainishwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Julai 12 mwaka huu
kijijini hapo na kusimamiwa na Afisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya
hiyo Bwana Kernslave Wensle Mpoto.
Pesa hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Idimi iliyoezuliwa Desemba 24 mwaka uliopita.
Aidha
imedaiwa kuwa Bwana Myola,amekuwa akiendesha kamati ya ujenzi wa shule
pekee yake hali iliyopelekea kuwepo kwa hasara na wananchi kugomea
kuendelea kutoa michango ambapo matarajio ilitakuwa kukusanywa shilingi
milioni 11.
Katika
Mkutano huo aliagizwa na Afisa Utumishi Bwana Mpoto kuzirejesha fedha
hizo na mifuko hiyo ya saruji katika mkutano wa hadhara ujao
utakaofanyika Julai 20 mwaka huu.
Hata
hivyo juhudi za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana
Yohana Bahati na halmashauri yake,zilishindikana baada ya tuhuma
zilizowasilishwa katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya kukosa nguvu za
kumtia hatiani.
Agizo
likatolewa kwa viongozi wa vitongoji kuhakikisha michango yote
inayochangwa na wananchi imewasilishwa kwa Afisa Mtendaji wa Kata kabla
ya tarehe hiyo iliyopangwa kwa ajili ya mkutano ujao wa hadhara.
0 comments:
Post a Comment