Na Ali Issa Maelezo Zanzíbar
KAMPUNI
ya simu za mkononi Zanzíbar ZANTEL imeahidi udhamini wa Shl. milioni
32 pesa taslimu kwa Kampuni ya Zanzibar Medium Corporación kwa ajili
ya tunzo ya wana muziki bora wa Zanzíbar mwaka 2012.
Udhamini
huo umetangazwa leo na Mkurugenzi wa Biashara Zantel upande wa
Zanzibar Mohammed Mussa wakati akizungumza na wandishi wa habarí
katika ukumbi wa Idara ya Habarí Maelezo mjini Zanzíbar.
Amesema
pesa hizo zimetolewa kwa ajili ya kudhamini tunzo hiyo ikiwa ni njia
moja wapo ya kuthamini na kuheshimu mchango ambao wanamuziki wa
Zanzíbar wamekuwa wakiutoa ikiwa ni pamoja na kuielimisha na
kuiburudisha jamii.
Ameongeza
kuwa Kampuni ya kizalendo ya Zantel imekuwa ikitoa huduma zake na
kujenga mapenzi ya dhati kwa jamii ikiwemo kujenga visima vya maji sita
ili kuhakikisha faida inayopatikana inaifaidisha jamii kwa ujumla
Mkurugenzi
huyo alisema pesa hizo zitatolewa kwa kuzingatia misingi imara na
kuepuka upendeleo na kwamba Zanzitel itaendelea kuwa karibú na jamii
kwa kutoa ushirikiano pale ambapo itahitajika.
Kwa
upande wake Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Zanzibar Medium
Corporación ambao ndio waandaaji wa tunzo hiyo Said Khamis aliishukuru
kampuni ya Zantel kwa kudhamini tunzo hizo na kuiomba indelee kuwa
karibú na jamii pale ambapo watahitajika kutoa msaada wao.
Aidha
amefahamisha kuwa tunzo hizo ambazo zitatolewa zitakuwa zimegawika
katika makundi 16 ya aina mbali mbali za wasanii ikiwemo makundi ya
muziki wa kizazi kipya (Zenji Fleva) na Taarab asilia.
Tamasha
hilo la saba litafanyika Bwawani siku ya Ijumaa,Juni 6 mwaka huu
ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilali .
0 comments:
Post a Comment