Rais wa shirikisho la soka nchini
TFF Leodger Chilla Tenga
=====
Na Shaban Kondo,
Serikali imekubali
mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la soka nchini TFF uendelee kwa sharti la
kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi
iliyo chini ya mwanasheria Iddy Mtiginjola.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa baada
ya kikao kilichoketi jana kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF pamoja na
Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Amesema baada ya makubaliano
hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la soka duniani FIFA ambalo lilisimamisha
mchakato wa uchaguzi mwezi uliopita kwa ajili ya kutuma ujumbe ambao unatarajia
kuja nchini kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.
Katika hatua nyingine
raisi Tenga amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu
kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.
Rais Tenga amewakumbusha
wanachama wa TFF ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu wanaopita mikoani kuomba
saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano
ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA.
Wakati huo huo
mwenyekiti wa baraza la michezo la taifa BMT Dioninz Malinzi ambae
aliuwakilisha upande wa serikali katika mkutano na waandishi wa habari amesema
hawana shaka na maafikiano yaliyofikiwa baina yao, lakini kikubwa akasisitiza
taratibu walizoagiza zinastahili kufuatwa za kuwatendea haki walioenguliwa
kwenye mchakato wa uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment