Pages


Home » » Ang'atwa pua na kupoteza kiungo hicho wakati akidai pesa zake shilingi 2,500/= Mkoani Mbeya.

Ang'atwa pua na kupoteza kiungo hicho wakati akidai pesa zake shilingi 2,500/= Mkoani Mbeya.

Kamanga na Matukio | 05:20 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
  Jamu Mwakyoma mkazi wa kijiji cha Isange kata ya Isange wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amejikuta akipoteza pua yake baada ya kukang’atwa wakati wa ugomvi akidaiwa shilingi elfu mbili mia tano.



Katika ugomvi huo Jamu Mwakyoma alikuwa akigombana na Zawadi Mwalije baada ya watu hao wawili kudaina fedha kiasi cha shilingi elfu mbili mia tano kwa kipindi kirefu.



Nao baadhi ya mashuhuda wamesema kitu kilichochangia ugomvi huo ni ulevi kutokana na wote wawili kuonekana kuwa wamekunywa pombe kupita kiasi.



Mwenyekiti wa kijiji hicho Lutengano Mwakyoma amesema baada ya tukio hilo Zawadi Mwalije amekamatwa kwa hatua zaidi za kisheria kutokana na kumjeruhi vibaya mwenzake.

Wakati huohuo Mwalimu Ahadi Mwandeko wa Shule ya Msingi Motomoto, Kata ya Ruiwa, Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa ameng'atwa mkono wake wa kulia na nyama kunyofolewa na mwanamke mmoja tukio lililohusishwa na imani za kishirikina.

Kwa mujibu wa Mwalimu huyo amesema siku ya jumamosi aliingiliwa na mwanamke jina linahifadhiwa na kung'atwa mkono wake na kutokomea kusikojulikana na alipoamka asubuhi alikuta nyama hakuna katika mkono wake wa kulia ndipo alipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Kassim Mwagala ambaye naye alilazimika kuitisha mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo mwanamke aliyetuhumiwa aliulizwa juu ya kitendo hicho alishindwa kujieleza hali iliyopelekea kuzomewa na wananchi na kumtaka airudishe nyama hiyo na kutakiwa aondoke mara moja kijijini hapo na inadaiwa alitokea katika kijiji cha Malamba.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Motomoto Bwana Mwagala amefanya kazi ya ziada ya kumficha mwanamke huyo baada ya wananchi wa kijiji hicho kutishia kumzika mwanamke huyo akiwa hai..

Katika tukio jingine Abel Mwasile amekutwa amefariki dunia katika mfereji karibu na reli ya TAZARA na chanzo cha kifo chake kimetokana na kunywa pombe kupita kiasi na tukio hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho na kueleza kusikitishwa na kitendo cha wananchi kushindwa kutoa taarifa hali iliyopelekea mwili wake kuharibika.    
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger