Timu ya Taifa ya
Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa
ndege ya Emirates tayari kwa mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za
kombe la dunia za mwaka 2014, dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars
uliopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa taifa jijini Dar
es salaam.
Afisa habari wa TFF
Bonifas Wambura amesema msafara wa timu hiyo utakaokuwa na watu 58 wakiwemo
maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam majira ya saa 8.55 mchana na
utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Wachezaji walioko
kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kilicho chini Kocha Rachid Taoussi
ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif
Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich
na Abdeljalil Jbira.
Issam El Adou, Kamel
Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine
Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah
Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El
Arabi.
0 comments:
Post a Comment