Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia
wahamiaji haramu wanne raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume
cha sheria.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakiel
Masaki amesema watu hao wamekamatwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati
ya polisi na madereva Tax wa maeneo ya Uyole.
Amewataja waliokamatwa kuwa ni Tarafa Mgomewa mwenye umri wa miaka 18, Mlegeta Tadesa mwenye umri wa
miaka 18, Damaka Lama mwenye umri wa miaka 20 na Nighato Tagenya, mwenye umri
wa miaka 22 wote raia wa Ethiopia.
Aidha watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano na jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment