·
Aoa Mwanafunzi wa kidato cha pili kwa Ng’ombe 45.
·
Atishia kuua wanaomfuatilia.
·
Mwanafunzi arudishwa kwa wazazi wake kukwepa
mkono wa Sheria.
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha
Mpona Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya anatuhumiwa kumwachisha
masomo mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Totowe kwa kumuoa
kisha kumpa ujauzito.
Mwananchi huyo aliyefahamika
kwa jina la Shigala Mwachanya anatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumpa ujauzito
mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Ngolo Jiguma(19) ambaye amesitisha masomo
yake kutokana na ujauzito alionayo ambapowazai walipatana kulipana Ng’ombe 45
kama fidia ambapo tayari Ng’ombe 20 wameshatolewa.
Aidha kutokana na Mwanafunzi
huyo kutambua kuwa Wazazi wake wametenda
kosa ameamlia kuto hudhulia kliniki katika kituo cha afya cha Malangali na
badala yake amekuwa akienda katika Zahanati ya Totowe ili kukwepa kukutwa na
vyombo vya sheria.
Uongozi wa Kijiji hicho umeanza kulifuatilia sakata hilo
baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule aliyokuwa akisomaMwanafunzi
huyo Frank Mwakisyala ambapo juhudi hizo zinaonekana kugonga ukuta kutokana na
kutishiwa kuawa na mtuhumiwa.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho
Yaledi Mwanguku aliwaambia waandishi wa Habari kuwa suala hilo lipo juu ya
uwezo wake hivyo alilazimika kulipeleka suala hilo kwenye uongozi wa kata kwa
ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Diwani wa Viti Maalumu kata
hiyoChristina Kibwana ambaye alionekana kulipokea suala hilo na kuanza
kulifuatilia pia alidai kuwa alipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukimtaka ahame
kijijini hapo lasivyo aache kulifuatilia sakata hilo na asipoachaangeuawa.
Diwani huyo alisema ujumbe huo
wenye maneno ya kutishia yalikutwa kwenye barua nje kidogo nje ya nyumba yake
ambapo aliongeza kuwa baada ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika
kituo kidogo cha Polisi cha Galula
Wilayani Chunya.
Diwani huyo aliendelea
kulalamika kuwa baada ya kutoa taarifa katika kituo hicho hakuna dalili wala
hatua zozote zilizochukuliwa ambapo alisema kuna dalili za Rushwa ambayo inasemekana
kuwa Polisi walipewa Rushwa ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(1500,000/=).
Alisema kutokana na kutoonekana
kwa hatua zozote aliamua kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya
Chunya ambapo walimkamata mtuhumiwa huyo kisha kufunguliwa kesi katika Mahakama
ya Wilaya ya Chunya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata
ya Totowe kupitia Chama cha Mapinduzi, Godian Wangala alithibitisha kutokea kwa matukio yote hayo
na kuongeza kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mwananchi huyo pamoja na wazazi
kwa kumwachisha masomo na kumsababishia Mwanafunzi kumnyima haki ya kupata
elimu.
Alisema Elimu ni haki ya msingi
ambayo ingeweza kumkomboa kifikra na Serikali kufikia malengo yake ya kutoa
elimu kwa wote kwa kuhimiza ujenzi wa shule za kata na kuongeza kuwa Mwanafunzi
huyo amekuwa akiyumbishwa kutokana na kukatishwa mahudhurio ya Kliniki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Diwani Athumani amekiri kupokea taarifa
hizo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha wahusika
watachukuliwa hatua zinazostahili.
0 comments:
Post a Comment