Mahakama kuu Kanda ya
Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha
miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila
kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma mashtaka mbele ya jaji
wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole
alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha
195 (16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Ngole aliiambia Mahakama hiyo
kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku
ambapo alifika nyumbani kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na
baadaye kuidondosha sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja walioathirika na moto
uliokuwa umewashwa kutokana na sigala
aliyokuwa ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni
Daniel Mwang’ombe, Anitha Richard, Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson,
Maria George na Cloud Samson.
Kutokana na kosa hilo mtuhumiwa
huyo alikiri kuhusika na kwamba aliua bila kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa
anavuta sigala alidondosha kipande hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha Mwendesha huyo aliiambia
mahakama hiyo kuwa pamoja na mtuhumiwa kukiri kusababisha vifo bila kukusudia
mahakama impe adhabu kali kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu
hiyo Wakili wa upande wa utetezi Sambwee
Shitambala alisema Mahakama inatakiwa
kumwonea huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa kutokana nay eye kuwa miongoni mwa wafiwa.
Alisema mshtakiwa ameondokewa
na wazazi, watoto na mke katika ajali hiyo ambapo hakuhudhuria mazishi yao pia
amekaa muda mrefu akiwa mahabusu ambapo
amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa ni kijana ambaye ni nguvu
kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Hata hivyo kutokana na utetezi
huo Jaji Karua alisema kutokana na hali iliyojitokeza mtuhumiwa atatumikia
kifungo cha miaka mitano kwa kila tukio ambalo ni kusababisha vifo saba hivyo
jumla atatumikia miaka 35.
0 comments:
Post a Comment