Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wananchi
wa kitongoji cha Mkulila kijiji cha Wambishe kata Ulenje wilaya ya Mbeya Mkoani
hapa wamekataa mradi wa umwagiliaji uliopelekwa na serikali kwa madai kuwa
hawakushirikishwa wakati wa uanzishwaji wa mradi huo ambapo pia wamesema
hawaoni faida ya kuwa na mradi kama huo kijijini hapo.
Mradi ni kwa ajili ya umwagiliaji ulioletwa na serikali kwa gharama ya shilingi zaidi ya milion 40 ambapo wananchi hao wamedai kuwa mradi wa maji hautawasaidia chochote kutokana na kuwepo kwa mfereji unaotiririsha maji kwa kipindi chote cha mwaka.
Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ulioitishwa na Ofisi ya Wilaya kwa lengo la kuwaelimisha wananchi hao juu ya faida ya mradi huo jinsi utakavyowanufaisha kama kijiji na wananchi kwa ujumla.

Pamoja na
Maofisa hao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mradi walipinga vikali
huku wakidai fedha za meadi huo zipelekwe sehemu nyingine zakafanye kazi
zingine.
Mkutano
huo uliokuwa ukiongozwa na Maofisa Umwagiliaji kutoka Ofisi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mbeya ambao ni Malonga Msuya na John Kajange walijikuta katika wakati
mgumu kutokana na mwitikio hafifu wa wakazi.
Hata hivyo
Diwani wa kata hiyo Noel Mwankwale aliwasihi wananchi hao kuwa wasikivu na
kuukubali mradi huo lakini pia juhudi zake ziligonga ukuta baada ya wakazi hao
kuendelea kusisitiza kuwa hawautaki kabisa.
Walisema fedha
hizo ni nyingi na kwamba haziwezi kutumika kujengea mfereji ambao hauna tatizo
walamanufaa kwao kutokana na kutiririsha maji muda wote.
Miongoni mwa
watu waliozungumza katika mkutano huo na kuukataa mradi ni pamoja na chifu wa
eneo hilo Michael Mwaifwani ambaye alisisitiza kuwa yeye kama chifu hajaona
tatizo lolote katika mfereji huo.
Mmoja wa wakazi
hao Christian Matengere ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyeondolewa
alisema ni vema wananchi wakasikilizwa na kutendewa vile wanavyotaka na siyo
kuwalazimisha.
Alisema pia
anasikitika kuona Serikali kutorudisha
fedha zake alizokuwa ametoa kwa ajili ya kufungua akaunti ya benki kwa ajili ya
mradi huo ambao alisema hauna maana yoyote.
Awali Maofisa
hao walisema lengo lao la kufika kijijini hapo ni kutoa elimu ambayo walikuwa
wakiilalamikia kwamba hawakuipata kuhusu mradi na manufaa ya mfereji na kwamba
hakuna shamba wala nyumba itakayoathirika wakati wa ujenzi wa mradi huo.
Aidha Mkutano
huo ulifungwa pasipo kufikia muafaka wowote
licha ya wananchi kuendelea kusisitiza kutouhitaji na kushauri kuwa
mradi huo upelekwe kijiji cha jirani che uhitaji wa maji na sio wao.
0 comments:
Post a Comment