Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Halmashauri
ya jiji la Mbeya imetoa zaidi ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa vyumba 24 vya madarasa katika shule ya Sekondari Nzondahaki iliyopo
kata ya Nzovwe.
Akiongea
na Mwandishi wa habari hii Afisa mtendaji wa kata hiyo Furaha Malele amesema
fedha hiyo itasaidia kukamilisha vyumba vya madarasa 24 kati ya vyumba 32
vilivyopo kwenye shule hiyo.
Amesema
fedha hizo zitatumika katika kununua saruji kwa ajili ya sakafu na ripu, mbao
za kenchi, mabati ikiwa ni pamoja na kugharamia kupaka chokaa kwenye vyumba
vyote 24.
Wakati
huohuo ameahidi kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo ndani ya siku 7 ili
kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao katika hali nzuri.
0 comments:
Post a Comment