Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Asasi ya
Tehilah Foundation ambayo pia inamiliki Shule ya Sekondari ya Vanessa iliyoko
Isyesye Jijini Mbeya imetoa msaada wa fedha taslimu shilingi Milion 55 kwa
ajili ya watoto yatima 31.
Akikabidhi
Msaada huo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Vanesa Osward Mwachande, Mkurugenzi
wa Asasi hiyo Shukrani Mwasanjobe alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ada ya
watoto yatima 31 wanaosoma kidato cha kwanza na kuongeza kuwa ada hiyo
itawasaidia hadi kidato cha nne.
Alisema lengo
ni kupunguza wimbi la watoto yatima mitaani kutokana na wingi wa watoto hao
kuondokewa na wazazi wao kwa Ugonjwa wa Ukimwi ambapo wengi wao wamekuwa
watelekezwa na ndugu baada ya wazazi wao kufariki.
Aidha aliiomba
jamii nyingine kusaidia watoto hao upande wa michango mingine kama sare za
shule na madaftari ambapo yeye amelipia ada kwa miaka mine.
Pia aliwasihi
walezi wa watoto hao kuwahimiza kusoma na kuhudhuria masomo ili waweze kufaulu
kidato cha nne na kuendelea katika masomo ya juu ambako pia ni rahisi kupata
misaada kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema
watoto wanaonufaika na msaada huo wanatoka katika kata za Iyunga, Isanga,
Isyesye, Nzovwe na Mbalizi Road zote za Jijini hapa ambao wengi wao walifauru
kujiunga kidato cha kwanza katika shule za Serikali lakini hawakujiunga
kutokana na ukosefu wa ada.
Akitoa
Shukrani kwa niaba ya walezi wa watoto hao Mtendaji wa Kata ya Isanga Fideris
Mwaselela alisema mchango wa mkurugenzi huyo umeisaidia Halmashauri ya Jiji la
Mbeya ambayo ndiyo iliyokuwa na jukumu la kuwasomesha watoto hao.
Aliongeza kuwa
watoto hao wakifaulu vizuri ndiyo watakaokuwa wataalamu wa baadaye na kuisaidia
jamii na taifa kwa ujumla katika kazi za maendeleo.
Kwa upande
wake Ofisa Maendeleo ya Jamii kata ya Isyesye Jiji la Mbeya Rose Kitundu
alisema idara yake inamshukuru mkurugenzi huyo kwa kutatua tatizo lililokuwa
likiwakabili watoto hao.
Alisema jukumu
la kusaidia watoto hao ni la kila mtu ambapo aliongeza kuwa Mkurugenzi huyo
amewaokoa katika kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa kutokana na kuzurura
mitaani.
0 comments:
Post a Comment