Pages


MGOMO WA WALIMU,IMEKUWA FURSA KWA VIBAKA KUNUFAIKA - TUNDUMA - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:35 | 0 comments
Na: Ezekiel Kamanga,Tunduma
Kufuatia Mgomo wa walimu ulioanza jana, wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Mji mdogo wa Tunduma,Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya waliamua kuandamana ili kudai haki ya kufundishwa katika maandamano ambayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya mji huo na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.

Hatua hiyo ilijitokeza mapema saa 2 asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri wa Tunduma,walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani ambapo baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi cha mjini hapa kabla ya kufika ofisi za halmadhauri ya mji.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, awali wanafunzi hao walikwenda nyumbani kwa Diwani wa kata ya Tunduma mheshimiwa Frank Mwakajoka (CHADEMA) na baada ya kufanya mazungumzo na mke wa diwani huyo ambaye inadaiwa hakuwepo waliandamana hadi kituo cha polisi na kuelekea katika ofisi za halmashauri ya mji ambapo msafara huo uliingiliwa na baadhi ya watu walioendesha uporaji huo.

Mmoja wa shuhuda hao ambaye alijitambulisha kuwa ni Julius Edward, alidai kuwa baada ya wanafunzi hao kufika katika ofisi  za polisi walipokelewa na kufanya mazungumzo ambayo  maamuzi yake hayakuafikiwa na wanafunzi hao.

Alisema baada ya kutoafiki majibu yaliyotolewa na Polisi wanafunzi hao waelekea kwenye mzunguko wa barabara uliopo karibu na eneo la ofisi za Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika mpaka wa Tanzania na Zambia ambako walizuia barabara ili magari yasipite.

Usumbufu huo ulidaiwa kujitokeza kwa muda wa nusu saa, hatua ambayo ilisababisha polisi wa kituo hicho kufika eneo hilo na kulazimika kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia mabomu mawili ya machozi hali ambayo ilisababisha vibaka kujiingiza na kuaanza uporaji kwa kukimbilia ziliko ofisi za halmashauri ya mji.

Watu hao ambao wameonekana wakivamia ofisi hizo na kuchoma moto baadhi ya mali za halmashauri hiyo huku wakipora  kompyuta 5 za ofisi, pikipiki yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali sambamba na kuvunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya kubebea taka aina FAW  SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo  na gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.

Kulingana na tukio hilo vibaka wameweza kuonekana wakipora mali katika ofisi hizo huku wengine wakivunja chumba cha kuhifadhia mizigo mbalimbali na kufanikiwa kuiba mabati na viti na mali nyingi zilizokuwa zikibebwa,huku baadhi yao walionekana wamebeba madumu ya mafuta ya petroli wakitishia kuchoma jengo hilo.

Wanacnhi wa mjini hapa wanakumbuka matukio mbalimbali yanayojitokeza katika mji huu kuwa huwa yana leta adhari, kama ilivyo tokea katika matukio machache ya Februari 18, 2005 kufuatia wamachinga watano waliokamatwa Nakonde Zambia na mnao Septemba mosi hadi 3 mtu mmoja aliyefia  katika mahabusu ya Nakonde nchini Zambia.

Mji wa Tunduma umekuwa kinala cha  matukio ya vurugu  na uvunjifu wa amani linapotokea jambo lolote hali ambayo huchangiwa na   watu wanaojiita wana harakati kuongoza vikundi vya watu ambao huaribu na kupora mali za watu.

Mkurugenzi wa mji huu Aidan Mwanshiga alipotakiwa kuelezea uharibifu hu alisema kuwa   tadhimini ya uharibifu uliotokea inafanywa na taarifa rasmi itatolewa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akizungumzia tukio hilo alisema kuwa tukio hilo haliwezi kuvumiliwa kutokana na kuwa maandamano ya wanafunzi hayawezi kupelekea kuvunjwa kwa ofisi za serikali bali kuna watu ambao wametumia mwanya huo ili kupora mali.

Aidha Kamanda Diwani alisema mbali ya uharibifu wa mali za Mamlika ya mji wa Tunduma hakuna madhala mengine yaliyotokea ikiwa ni pamoja na majeruhi au vifo vilivyojitokeza.


Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Momba Bwana Abiud Saideya amesema amesikitishwa sana na kitendo cha uharibifu wa nyaraka na mali za serikali na kudai kuwa hizo ni mali za wananchi,hivyo atahakikisha wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka amesema leo kutakuwa na mkutano wa hadhara wa kuzungumzia vitendo vilivyofanywa na watu hao ambao wamesababisha hasara kubwa kwa halmashauri. 

Wakati huo huo katika Kata ya Vwawa wanafunzi wa shule za Ichenjezya na Haloli waliandamana hadi ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mbozi na baada ya maandamano hayo walirejea shuleni kwao kwa amani huku wakisindikizwa na Polisi.

Wanafunzi hao walidai kuwa walimu wao walifika shuleni lakini hawakuwa tayari kufundisha wakiwaambia kuwa hawatafundisha kwa vile wapo kwenye mgomo hivyo waliwashauri waandamane hadi ofisi za halmashauri kudai haki yao hiyo.

Vilevile habari kutoaka Jijini Mbeya zimeeleza Mbeya zimeeleza kuwa mgomo ulianza mapema jana asubuhi, ambapo walimu walifika shuleni na kusaini kitabu cha mahudhurio kisha kukaa kimya huku wakiawaacha wanafunzi wakilandalanda bila cha kufanya.

SIKU AMBAYO SERIKALI YA KIJIJI CHA IYOVYO ILIYOTOONDOLEWA MADARAKANI.

Kamanga na Matukio | 02:55 | 0 comments

 Jinsi alivyokuwa akiondoka mkutanoni Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyovyo,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Bwana Rashid Likuta mara baada ya kuvuliwa madarakani kwa kile kilichodaiwa kuwa anajihusisha na ufujaji wa pesa za kijiji wa zaidi ya shilingi laki nne na kutosoma taarifa za mapato na matumizi.
 Baadhi ya Wajumbe walioteuliwa kuchunguza ubadhilifu wa pesa za Kijiji cha Iyovyo,wakikamilisha taarifa kabla ya kuisoma.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakisikiliza kwa umakini mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyovyo,Bwana Rashid Likuta.akijitetea kuhusiana na tuhuma zinazomkabili..
 Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakisikiliza kwa umakini mkutano huo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iyovyo Bwana Njobeni,aliyepewa madaraka ya kukaimu nafasi ya Uafisa Mtendaji wa kijiji mara baada ya Serikali ya kijiji kutenguliwa madarakani kutokana na ufujaji wa fedha za kijiji..
 Diwani wa Kata ya Totowe mheshimiwa Godian Wangala,akiwasihi wananchi kuendelea kuchangia maendeleo licha ya Halmashauri ya Kijiji kuondolewa madarakani kutokana na ubadhilifu wa fedha za kijiji.
 Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi Bwana Michael Mwamlima,akitoa taarifa za kubaini ubadhilifu huo uliofanywa na uongozi wa kijiji katika mkutano wa kijiji.
Meza na viti vikiwa wazi baada ya viongozi wa kijiji kuvuliwa madarakani(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya).

UGALI WASABABISHA WANANCHI KUUMWA MATUMBO - MBOZI

Kamanga na Matukio | 02:52 | 0 comments
Na Esther Macha,Mbozi
Wakulima wa Kijiji cha Ichesa Kata ya Myovisi ,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya wamelalamikia kuumwa matumbo baada ya kula ugali unaodaiwa kutokana na mbegu feki ya  mahindi ya njano inayodaiwa kusambazwa na wakala mmoja kijijini hapo.

Kutokana na adha hiyo wakulima hao wameziomba mamlaka husika na watafiti kulifuatilia kwa kina suala la ununuzi wa vocha za mbolea ya ruzuku kutoka kwa wakulima kumuuzia wakala kwa bei ya kati ya sh.2,000 hadi Sh.4,000 unaodaiwa kufanywa na wakala mmoja jina limehifadhiwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ichesa (majina tunayo)walisema kuna hatari kubwa kwa mwaka huu waananchi wa Kijiji hicho kukumbwa na baa LA njaa na hali ya uchumi kushuka kutokana na kusambaziwa mbegu inayotoa unga wa njano inayodaiwa ya kampuni ya pannar na hivyo kukosa kabisa soko.

Bw.Nasibu Mwashilindi alisema wamejitahidi kwenda kuuza mahindi hayo kwa sh. debe sh.2,000 katika soko la mazao Mlowo licha ya bei ya mahindi kwa debe kupanda hadi kufikia sh.6,000 lakini hayanunuliwi na kurudi nayo majumbani.

"Hali ni mbaya ndugu zangu haya mahindi ni shida kwani hakuna anayenunua kutokana na ugali wake kuwa mchungu mdomoni na hata upande wa soko bado ni tatizo sana sisi wananchi wa kijiji cha Ichesa tuna wakati mgumu sana kwani uchumu wetu wa maisha ni mgumu kufuatia hali hii kwani hatujui haya mahindi tutayapeleka wapi mpaka sasa"alisema mwananchi huyo.

Bw.Mwashilindi alisema kibaya zaidi mahindi hayo hayaliki kutokana na uchungu wa ugali wake hasa ukipoa na wengine wanalalamika watoto wao kuumwa matumbo wanapokula jambo ambalo wamehofia kuwa linaweza kuleta athari kiafya.

Baadhi ya wakulima walifafanua kuwa mbegu hizo zilizokuwa rangi ya njano wameuziwa na wakala huyo ambapo mfuko umeonesha zimetoka katika kampuni ya Pannar lakini katika jambo la kushangaza hata kibunzi ni chekundu na imefikia hatua wananyanyapaliwa katika mashine za kusaga kama watu wenye kimela cha kutengenezea pombe.

"Tunapokwenda kusaga mashine wanatuambia tusubiri hadi wamalize kusaga wenye mahindi meupe na sisi ndiyo tunakuwa wa mwisho hata kama tumewahi,sababu ni kwamba nikitangulia mimi mwenye mahindi ya njano na wote watakaofuatia hata wakiwa na mahindi meupe yanabadilika kuwa njano,"walisema.

Akizungumzia malalamiko hayo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ichesa,Bw.Paul Mwasenga alisema walipokea vocha za ruzuku za pembejeo 600 za mbolea aina ya Urea ya kukuzia mwezi februari,2012 na kwamba kweli vocha za mbolea ya kupandia aina ya CAN hazikufika kabisa.

Bw.Mwasenga alikanusha kusikia taarifa ya wakala kununua vocha za ruzuku kwa Sh.2,000 amekanusha vikali na kudai hizo ni njama za kuchafuana kisiasa na hakuna kitu kama hicho ingawa alifafanua.

Mtendaji huyo amekiri kupata malalamiko ya kuwepo mbegu feki ya mahindi ambayo imekuja kubainika baada ya mahindi kukomaa na kwamba wakulima walinunua mbegu hiyo katika maeneo tofauti ikiwemo kwa wakala Ntandala wa Kijiji cha Ichesa ambaye ndiye alikuwa akisambaza Kata ya Myovisi.

Katika suala hilo wananchi walisema Wakala huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji aliwashawishi wananchi kumuuzia vocha ambazo zote alikuwa ameshazisaini kwa bei hiyo hali iliyowafanya baadhi ya wakulima kumuuzia baada ya kuona hazina umuhimu tena kutokana na mbolea aina ya Urea kuchelewa kufika na Can kutokufika kabisa ilhali mazao yameshaanza kukomaa.

Mjumbe wa kamati ya ugawaji wa vocha ya Kijiji cha Ichesa,Bw.Mashaka Mwashambwa alisema hajawahi kusikia madai hayo na kazi wanayoifanya kamati ni kubwa kwani kabla ya kugawa wanatoa elimu kuhusu thamani ya vocha na punguzo lililotolewa na serikali baada ya kuitisha mkutano wa hadhara na baadaye walitembelea mashamba na kugawa vocha kwa wahusika.

Hata hivyo wajumbe wengine watano kati ya sita akiwemo Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Vocha ya kijiji cha Ichesa hawakuweza kupatikana kuelezea sakata hilo.

Ofisa kilimo Kata ya Myovisi Bw.Danfod  Mandali   amethibitisha kupokea malalamiko ya mbegu feki  na hivyo alichukuwa hatua ya kuwasiliana na Ofisa wa kilimo Wilaya ya Mbozi ambaye alifika na timu ya wataalamu waliwahoji wakulima na kuchukua sample.

Bw.Mandali alisema  suala la madai ya baadhji ya wakulima kuuza vocha kwa wakala halijamfikia rasm,i ila kuna tetesi mitaani wakulima wakiwataja wenzao wanaolalamika kuuza kwa bei ya chini vocha hizo baada ya kuziona hazina kazi tena kutokana na mazao yao kukomaa.

"Wakulima ni kama asilimia 40 walioathirika na mbegu hiyo na kuhusu kuuza vocha  nimewahi kuwasikia wakulima wakiwataja wenzao waliouza kwa wakala huyo  lakini wanaficha ficha kuhofia kukosa kupata katika msimu unaokuja  kwa sababu kisheria ni makosa...huku ilikuja UREA tena kwa kuchelewa mwezi Machi,mbegu na mbolea ya kupandia walisema imehifadhiwa mkoani watapewa mwezi septemba, kwa ajili ya msimu wa 2012 na 2013,"alisema.

Wakala aliyedaiwa kugawa mbegu na kununua vocha katika kijiji cha Ichesa, Bw.Japhet Ntandala alipohojiwa kuhusiana na tuhuma hizo alikanusha na kulaani vikali kwamba wanataka kumchafua mbele ya wananchi wake na kwamba yupo tayari kununua mahindi yote kwa wale aliowauzia mbegu ili wananchi wake wasife na njaa.

Wakala huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji hicho alisema hajawahi kununua vocha na angependa mtu aliyedai amemuuzia ajitokeze ili azungumze ukweli na yupo tayari kufika naye mahakamani ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Mbeya ,Dkt.Philipo Mwaisoba alishukuru kupata taarifa hiyo na kuahidi kufuatilia huku akidai ni hatari kubwa endapo vocha za ruzuku zimeuzwa tena kwa wakala kwani ni makosa kisheria na kwamba atafuatilia kujuwa mbegu hizo zinazodaiwa feki na kutolea majibu.

Jitihada za kuwasiliana na Kampuni ya Pannar na watafiti,Mamlaka ya chakula na dawa zinaendelea ili kubaini jitihada zinazofanywa ili kunusuru maisha ya watu wa Kijiji cha Ichesa na maeneo mengine ya wilaya ya Mbozi ambayo yanadaiwa kusambazwa mbegu hizo feki.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa kuna taarifa ya kusambazwa kwa mbegu hizo feki karibu maeneo mengi ya Wilaya ya Mbozi na kuna hofu ya wananchi walio wengi kupata madhara ya kiafya na hali ngumu ya maisha kutokana na mahindi hayo kukataliwa na wanunuzi wa mazao.

UMUHIMU WA MAJI VIJIJINI NA MIJINI KWA WANANCHI

Kamanga na Matukio | 02:51 | 0 comments
Na Ester Macha.
Tunapozungumzia maji  kwa binadamu  ni pamoja na huduma hiyo kupatikana vijijini na mijini ambako mahitaji hayo ni muhimu kwa wananchi waishio maeneo  hayo lakini hali hiyo imekuwa tofauti kwa maeneo ya pembezoni na kujikuta wakiishi bila ya kupata huduma ya maji safi na salama.

Kutokana na hali hiyo  serikali ilitunga sera ya maji kwa kushirikiana na walengwa  kwa kubuni, kupanga, kujenga, kuendesha, kufanya matengenezo na kuchangia gharama za huduma utunzaji na usimamizi endelevu wa rasilimali za maji kwa kushirikisha wadau wote kwa kupunguza   majukumu ya utekelezaji kwa serikali ili kusimamia,kuratibu, kushauri, kuwezesha na kutoa miongozo.

Sera hiyo imekwenda tofauti kwa wananchi waishio vijijini na kusahaulika katika suala zima la maji safi na salama na kujikuta wakitumia maji machafu ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu ,lakini kutokana na shida ya maji hulazimika kutumia ili kuweza kukidhi mahitaji.

Muundo wa Sera  ya maji una sehemu kuu tatu za usimamizi wa rasilimali za maji kuweka na kuendeleza mfumo endelevu  na madhubutiwa kusimamia rasilimali maji Utoaji wa huduma ya majivijijini Kuboresha afya za wananchi wa vijijini, kuchangiakupunguza umasikini kwa kutoa huduma endelevu ya majisafi, salama na ya kutoshaUtoaji wa huduma ya majisafi na maji mijini Kuweka mfumo endelevu wa kutoa huduma kwa bei nafuu ili makundi yote yaweze kupata huduma ya maji.

Hivi karibuni timu ya wanahabari wanaharakati wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) walitembelea kijiji cha Ifiga kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya  kujua tatizo la maji katika kijiji hicho jinsi linavyoathiri uchunmi wa wananchi wa eneo hilo .

Uhaba huo wa maji umekuwa sugu katika eneo hilo na kupelekea kutumia maji ya visima  ambayo si safi na salama na kujikuta wakiendelea kukumbwa na magonjwa ya kichocho  hasa kwa watoto na watu wazima.

Akizungumza na gazeti hili Mkazi wa Kijiji chsa Ifiga Bi.Sophia James anasema kuwa kisima hicho wamekuwa wakitumia wakazi 2000 wa kijiji hicho na kuwa pamoja na kuwa maji hayo si salama baadhi ya watu hasa watoto wamekuwa wakiyanywa pasipo kuchemcha  na hivyo kukubwa na maradhi ya tumbo.

Hata hivyo Bi.James anasema kuwa kutokana na hali hiyo ya tatizo la maji kijijini bado wamekuwa wakichangia wa  mradi wa maji bila mafanikio na hivyo kuomba serikali kusaidia kutatua tatizo hilo bila mafanikio .

Anasema wanawake wa eneo hilo  na watoto wamekuwa wakiathirika zaidi na tatizo la ukosefu wa maji kutokana na kisima hicho kuwa mbali na makazi yao hivyo wakati mwingine kutumia muda wa masaa manne hadi 6 kwenda kutafuta maji Kisimani .

Mwanamke huyo anasema kuwa  kutokana na tatizo hilo la maji wanawake walio wengi wameshindwa kuwa wazalishaji wazuri kutokana na muda mwingi kutumia kutafuta maji kwa kwenda uymali mrefu.

Aidha Bi.James anasema kuwa  kuachiwa majukumu zaidi ya kulea familia kwa kufanya kazi ya kusaka maji pamoja na shughuli nyingine za shamba huku baadhi ya wanaume wao wakishinda katika vijiwe wakisubiri kuhudumiwa na mwanamke.

Mwanamke mwingine Sevelena Mwahewa anasema tatizo la maji katuika kijiji cha ifiga ni kubwa  utokana wao kutembea umbali mrefu kutafuta maji ambako hata hivyo wakifika kunakuwa na foleni kubwa ambayo huwalazimu kusubiri kwa kupanga foleni.

“Tukiwa huko Kisimani inatubidi kukaa na kusubiliana kwa muda mrefu ambapo baada ya kuchelewa kurudi nyumbani waume zetu hutupiga na kuhoji tulikokuwa na kutoamini kama tulikuwa kisimani kusubiri maji,kwa ujumla hili ni tatizo kubwa kwetu  mimi mwenyewe ni moja wapo wa wanaume wa wanawake ambao nimepata kipigo kutokana na kuchelewa kurudui nyumbani”anasema Sevelena.

Hata hivyo anasema kuwa mara baada ya kupata vipigo hivyo kutoka kwa waume zao hushindwa kushtaki popote kutokana na kutishiwa na waume zao kuwa wasiseme popote . tatizo hili la maji limepelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kijini hapa.

Anaongeza  kuwa hata ukijaribu kumpeleka mahakamani mwanaume  jamii inayowazunguka humtenga mwanamke aliyemshtaki mumewe kuwa ni aibu kufanya hivyo.

Naye  Anna Mbalawala  Mkazi wa Ifiga anasema kuwa tatizo hilo la maji limeanza kujitokeza kati ya mwaka 2007 baada ya uongozi wa Halmashauri ya mji wa Mbeya kuanza mchakato wa kuwa jiji na hivyo kulazimika kuchukua mradi wa maji ambao ulichangiwa na wananchi wa kijiji hicho pia kwa kuchimba mtaro wa maji kutoka kijijini hapo na maji hayo kwenda kutumiwa na wakazi wa jiji la Mbeya.

Mwanamke Mwingine Bi.Frola Mlowezi anasema kuwa wananchi wa kijiji hicho kutumia maji ya kisima ambayo si salama watoto wake wawili wamekuwa wakitibiwa ugonjwa wa kichocho mara kwa mara kutokana na kutumia maji hayo ya kisima.

“Hii hali kwa kwali ni mbaya hapa kijijini kwetu tunaomba uongozi husika kutusaidia tatizo hili ili tuweze kupata maji ambayo ni salama vinginevyo hali hii inaweza kuwa mbaya kwa watoto wetu maji haya ya kisima ni machafu tunatumia basi tu hatuna jinsi”anasema.

Hata hivyo anasema aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo Bw. Molis Selema anasema kuwa kabla ya mradi huo kuchukuliwa na jiji mwaka 2007 kulikuwa na kamati ya watumiaji maji ambayo kwa sasa ilivunjwa baada ya jiji kuchukua mradi huo.

Akizungumzia adha hiyo ya maji Mwenyekiti wa kijiji cha Ifiga Bw.Raphael Syejele anasema ni kweli tatizo hilo  maji lipo kijijini hapo alithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo la maji kijijini hapo na kuwa ugonjwa huo wa kichocho unachangiwa na huduma mbaya ya maji wanayotumia wananchi wake .

Anasema kijiji cha Ifiga kina wakazi 1175 wakiwemo watoto 748 na wazee 127 anasema kati ya wakazi wa kijiji hicho 636 ni wanawake ambao ndio wamekuwa wakitegemewa zaidi katika familia kwa kutumia kutafuta huduma hiyo ya maji.

Kuhusu kijiji cha Iwalanje wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa ni miaka 14 sasa hawajawahi kupata maji mpaka sasa licha ya kuendelea kuchangia maji,lakini hakuna mafanikio yeyote .

Bi. Marge John mkazi wa Iwalanje anasema kuwa wao wanailamu serikali kwani tuliambiwa tutachangie  asilimia 5 na tukakubali  lakini mpaka sasa hakuna dalili ya kupata maji mpaka leo.

“Tukiuliza kwa viongozi  wa vijiji  na kata  wanasema  wanafuatilia lakini kuna kipindi  Fulani walisema wakandarasi wamekosea kuchimba kisima cha maji hivyo bado tunasubiri”anasema.

Anasema kuwa maji wanayotumia wanachota Mto Shokwi  ambako hutoka saa 12 asubuhi na kurudi saa saba mchana  ambapo anasema hata hivyo katika Mto huo kuna Nyoka mkubwa aina ya Chatu ambaye ni hatari kwa maisha ya wanawake ambao ni tegemeo kwa familia.

 Aidha Mhandisi wa maji wilaya ya Mbeya Eng .Bahati Haule anasema kuwa bado serikali haina mpango wowote katika kijiji hicho kwa sasa katika kutatua kero ya maji wakati baadhi ya vijiji vya Iwalanje  vipo mbioni kutatua kero ya maji unafanyika.


Eng .Haule anasema kuwa hali ya upatikanaji wa maji safi kwa sasa katika Halmashauri ya Mbeya upo chini asilimia 50 na kusaema kuwa ipo mipango mbali mbali ya kutatua tatizo hilo baadhi ya maeneo huku akidai kuwa mbali ya kijiji cha Ifiga kutumia maji ya kisima bado kijiji cha Iwalanje pia wanatumia maji ya kisima.

Anasema kuwa Halmashauri imepokea fedha kutoka benki ya Dunia zaidi ya mil.800 kwa ajili ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Iwalanje na kusema kijiji cgha Ifiga wanasubiri wahisani waweze kusaidiwa .

Eng.Haule anasema kuwa maeneo ambayo yana matatizo ya maji katika wilaya ya Mbeya ni Mshewe ,Ipwizi,Chang’ombe,Mapogoro pamoja na Chelenje, Ifiga ambapo anasema utaratibu unaendelea ili maeneo hayo yaweze kupata maji.

HAKIMU ATOKA NJE YA MAHAKAMA NA KUZICHAPA KAVU KAVU NA MWANANCHI.

Kamanga na Matukio | 05:22 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Iyula Mbozi.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo,Kata ya Iyula,Tarafa ya Iyula,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Mheshimiwa Grace Kivelege aliuacha Ukumbi wa mahakama hyo na kutoka nje kisha kuanza kuzozana na mwananchi mmoja Bwana Sebastian Kilindu aliyekuwa amefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi.

Sababu ya ugomvi huoni pale Hakimu huyo alipomtaka mshitakiwa Bwana Laurence Julias,kuingia mahabusu ndipo Bwana Kilindu alipinga hali iliyompelekea hakimu kumkunja shingoni na kuamuliwa na mwandishi wa habari hizi,huku wananchi wakishangilia zogo hilo wakitaka Hakimu apigwe kutokana na kinachodaiwa kuwa kajijengea mazingira ya rushwa.

Baada ya kuamuliwa hakimu huyo alimfuata tena Bwana Kilindu na kumkunja mbele ya Kituo cha Polisi cha Iyula,Wilayani Mbozi huku akiporomosha matusi ya nguoni na kushangaza wananchi baada ya kuzivunja sheria ili hali kapewa dhamana ya kuzisimamia.

Aidha,kesi hiyo iliyokuwa ikimhusisha Bwana Laurence ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na baadae kukata rufaa katika Mahakama ya wilaya ya Mbozi na kuachiwa huru lakini alibambikiziwa kesi nyingine akidaiwa kuwapiga wananchi watatu wanaoishia katika Kijiji cha Ichesa wilayani humo.

Mtuhumiwa Laurence amekuwepo jela kwa muda wa mwezi mmoja,ambapo ndugu na jamaa walifika siku ya Jumatatu Julai 23 mwaka huu kwa ajili ya kuomba kumwekea dhamana ambapo Hakimu huyo Bi.Kivelege alikataa na kuwataka wafike siku inayofuata Julai 24 wakiwa na barua ya udhamini.

Aidha,walipofika siku hiyo Julai 24 mwaka huu wakiwa na barua ya udhamini,bado hakuwasikiliza hadi ilipofika majira ya saa 9:30 alasiri ndipo alipotoa hati ya kumtoa gerezani na mshitakiwa kufikishwa Kituo cha Polisi cha Iyula majira ya saa 12:30 jioni na kudhaminiwa na kaka yake mbele ya Mkuu wa kituo hicho Mkaguzi msaidizi Inspekta Uziweli Mwanga ambapo alitakiwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili.

Julai 25 mwaka huu mshitakiwa alifika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili lakini kabla ya kesi Bwana Laurence Julias aliwasilisha barua yenye sababu ya kumpinga hakimu huyo,ambapo sababu ya kwanza akidai hana imani naye, ya pili yupo karibu na walalamikaji na mwisho alidai kwamba kesi yake aliomba kutosikilizwa na hakimu huyo ambaye alitoa hukumu ya kwenda jela miaka mitatu bila sababu ya msingi.

Kufuatia hali hiyo Hakimu Bi Kivelege alionekana kukasirishwa na barua hiyo,hivyo kumtaka mshitakiwa adhaminiwe upya na kumamuru Mkuu wa Kituo cha polisi kumweka mahabusu hali iliyowakasirisha ndugu zake na kuleta tafrani kubwa katika kituo hicho.

Hata hivyo baada ya kuona hali hiyo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi Inspekta Mwanga alimrejesha Bwana Laurence mahakamani ndipo zogo lililopoanza,hakimu akitaka dhamana ya awali ifutwe huku sababu za kufutwa hazikuwekwa bayana.

Wakati huohuo Hakimu hakuendelea na kesi huku akiondoka na gari yake akiacha kesi nyingine bila kusikilizwa lakini katika uchunguzi uliofanya ulibaini kuwa jumla ya kesi 9 zilizohukumiwa na hakimu huyo zimekatiwa rufaa kutokana na watuhumiwa kuachiwa huru mahakama ya wilaya hali inayotia shaka utendaji kazi wake.

SERIKALI YAOMBWA NA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFANYIA UCHUNGUZI MADINI YA KULAMBA NA MIFUGO.

Kamanga na Matukio | 03:18 | 0 comments
*Habari na Ester Macha,Mbeya.
Wakulima na Wafugaji wa Kijiji cha Itizi,wilaya ya Mbeya Vijijini wameiomba Serikali kufanya uchunguzi kuhusu aina ya madini yanayodaiwa kuchakachuliwa na hivyo kusababisha asilimia kubwa ya ng’ombe kutokuzaa kwa zaidi ya miaka miwili sasa licha ya mifugo hiyo kulamba madini,kupata joto na kupandishwa.

Wamesema kuwa wameshindwa kuendelea kujenga mitambo ya Biogesi kutokana na kuhofia mradi huo kumalizika mapema na kukosa ruzuku,inayotokana na mradi unaofadhiliwa na Programu ya uenezi wa mitambo ya biogesi ngazi ya Kaya Tanzania (TDBP) chini ya Camartec kwa wakulima wanaojenga.

Wakizungumza na gazeti hili wakazi wa kijiji cha Itizi Bw.Anyesile Mwasanga na Alex Elias walisema wamekuwa wakizingatia kanuni za ufugaji bora kama walivyofundishwa na kuendelea kusisitizwa na mtaalamu wao wa mifugo kwa kulisha vizuri na wengine kufikia hatua ya kukaa na dume la ng’ombe nyumbani kwa zaidi ya siku tatu kutegea kabla ya muda wa kupata joto na kupandisha lakini hakuna matokeo yeyeote ya kushika mimba.

Hata hivyo wamebainisha kuwa  wana hofu kubwa ya kufanyika hujuma ya uchakachuaji wa madini kama ya awali kwani jiwe la madini limekuwa likikatika ovyo wakati wa kulamba ng’ombe na kumeguka ovyo. 

‘Tunajuwa umuhimu wa kutunza na kufuga ng’ombe kwani wanatuletea faida kubwa ya maziwa,ndama na kupata fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha na tunazingatia maelekezo ya mtaalamu lakini jambo hili limetushtusha sana mfugaji kukaa na ng’ombe wawili tu kwa muda wa miaka sita hadi saba hawakamati mimba,"alisema.

Bw.Acley Sauzan,Adamu Malankali na Imanueli Anangisye walisema wamekuwa wakifuata ratiba ya kupata joto ndani ya siku 18 na wanapata joto kwa haraka na kumpandisha dume lakini ni zaidi ya miaka miwili hakuna matokeo yeyote ya kushika mimba jambo ambalo linawanyima raha na kuwakatisha tamaa ya kuendeela kufuga na hivyo wameiomba serikali na mamlaka zinazohusika kufuatilia suala hilo.

Kwa upande wake Ofisa ugani na msimamizi wa mradi Caritas Mbeya,Bw.Hansley Hansley alisema tatizo hilo kitaalamu linaweza kusababishwa na ukosefu wa madini ama kutozingatia ratiba ya kupandisha ng’ombe na kwamba upo umuhimu wa kukaa na wakulima kujaribu kuangalia chanzo cha tatizo sanjari na njia ya kuzuia na kutatua.

Mkurugenzi wa Caritas Mbeya  Bw,Edgar Mangasila ametoa mwito kwa wakulima kuchukuwa jukumu la kuwaita wataalamu mara kwa mara kuzungumzia masuala mbalimbali yanayowakabili mapema badala ya kusubiri kupatwa na tatizo.

"Waiteni wataalamu wa Halmashauri,caritas na wengine kuzungumzia masuala yenu mbalimbali na siyo kusubiri hadi mmepata tatizo kwani mtakuja kujikuta mmepata hasara kubwa,Ninyi ndiyo mabosi wa wataalamu na mashirika yanayowasaidia kwa hiyo waiteni siyo hadi waamue wenyewe kuja..haya mambo yanahitaji ushirikishwaji,"alisema.

Alisema wakulima wasitegemee ndama na maziwa pekee bali waangalie manufaa mengine yatokanayo na ng’ombe mathalani teknolojia mpya ya bayogesi kwa kujenga mitambo ya bayogesi sanjari na samadi ambayo inarutubisha ardhi na hivyo wakulima watajikuta wakisahau suala la Vocha za ruzuku na kuacha kufikiria maduka ya mbolea.

"Ukibaki na ndama na maziwa maumivu yake ni makali lakini ukiingia katika bayogesi itapunguza maumivu kwa sababu mama atapikia,watoto watasoma kwa ajili ya mwanga,utapata maziwa kidogo ya lishe na watoto, na kinyesi hicho hicho kitatumika kama dawa ya kuuwa wadudu  katika mboga mboga,"alisema.

Hata hivyo Mangasila amewaondoa hofu wakulima hao kuwa mradi wa bayogesi unaendelea kwa miaka mitatu na hivyo ametoa wito kwa wakulima kuchangamkia mradi huo mapema kwani kadri siku zinavyozidi kusonga mbele na gharama za ujenzi zinazdi kuongezeka.

MWANANCHI ATAKAYEHARIBU VYANZO VYA MAJI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

Kamanga na Matukio | 03:16 | 0 comments

 Mh. Rais Kikwete akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi na upimaji wa maji katika Kijiji cha  Swaya,Wilaya ya Mbeya vijijini Julai 22 mwaka huu. 
********* 
Na Bosco Nyambege Mbeya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itamchukulia hatua kali za kisheria  mwananchi yeyote atakayebainika kuharibu  vyanzo vya maji nchini. 

Onyo hilo limetolewa hivi karibuni  na Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,alipokuwa akizindua mradi wa maji safi na upimaji wa maji katika Kijiji cha  Swaya,Wilaya ya Mbeya vijijini Julai 22 mwaka huu. 

Amesema uharibifu wa vyanzo vya  maji hupelekea kukosekana kwa maji na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kwa binadamu kama vile ukame,magonjwa pamoja na vifo. 

Aidha amesema ili kuthibiti tatizo hilo la uharibifu wa miundombinu ya maji ni vema kila mtu akahusika kulinda vyanzo vya maji vinavyomzunguka, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka husika waharibifu wa vyanzo vya maji wanapobainika.

Amebainisha kuwa serikali itahakikisha inatatua tatizo la uhaba wa maji hapa nchini ili kumwezesha mwananchi wa kipato cha chini kupata maji safi na salama kwa wakati muafaka. 

Mbali la hilo Rais  Kikwete amewasihi wananchi kulipa bili za maji kwa wakati muafaka ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi na wakati.

Mradi huo wa maji umegharimu kiasi cha shilingi 79.5 bilioni mpaka ulipokamilika na unatarajia kuhudumia watu zaidi ya laki tatu mkoani mbeya  kwa muda wa miaka mitano ijayo. 

Mradi huo umejengwa kwa udhamini kutoka Ujerumani,umoja wa ulaya-EU kwa Ushirikiano na serikali ya Tanzania mpaka kukamilika kwake.

UGOMVI ULIOKUWA UKIHUSISHA PANDE MBILI ZA FAMILIA YA MAREHEMU WASULUHISHWA,.

Kamanga na Matukio | 01:42 | 0 comments

 Sehemu ya mabati 57 yaliyotolewa na Familia ya Mligula iliyokuwa ikigombea mali za marehemu Eva Emmanual Mligula na Emmanuel Mwaigaga na kutoa vitisho kwa njia ya mtandao kwa Bwana Allan Mwaigaga,ambaye aliitaka familia hiyo kuchangia maendeleo ya Shule tatu za Msingi ya Itewe,Pankumbi na Mwashoma.
Viongozi wa kikabila(Machifu) na wanafamilia wa pande zote mbili za marehemu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza tofauti zao.(Picha na Ezekiel Kamanga)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Ugomvi wa kugombea mali za marehemu uliokuwa unahusisha familia mbili za marehemu Eva Emmanuel Mligula(38) na Emmanuel Mwaigaga aliyefariki miaka nane iliyopita waliokuwa wakiishi Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya umesuluhishwa baada ya familia hizo kukutanishwa na uongozi wa kimila na Serikali.

Awali ugomvi ulianza Julai 13 mwaka huu katika mazishi ya Mjane Eva,kufuatia Baba na kaka wa marehemu huyo kuwazuia ukoo wa Mwaigaga(kiumeni) kutokuwepo katika msiba na kutohudhuria mazishi kwa kile kilichodaiwa kuwa ukoo unaweza kuuza nyumba ya marehemu.

Mvutano huo ulielekea ukoo wa marehemu kubeba kila kitu kilichokuwemo ndani zikiwemo samani kwa kutumia gari yenye nambari T 788 BLK aina ya Fuso na T 314 AVA aina ya Center na kusababisha Bwana Allan Mwaigaga(Mwaji Group) kutoka ukoo unaotuhumiwa kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Uyole.

 Mkuu wa kituo hicho cha polisi Lazaro Kiyeyeu alifika eneo la tukio na kushuhudia vyombo vikibebwa na ukoo wa Mligula naye kwa kushirikiana  na Mwenyekiti wa mtaa Bwana Michael Mwamahondya kuchukua jukumu la kumtaarifu Diwani wa kata ya Uyole Bwana Ngambi Ngela ambaye aliwasihi wananchi waliokuwepo msibani hapo kurudi makwao na hivyo na kila familia ya marehemu kwenda kulilia msiba nyumbani kwao na nyumba hiyo ya marehemu kufungwa na yeye kukabidhiwa funguo kukabidhiwa Bwana Mwaigaga.

Aidha .baada ya funguo hizo kukabidhiwa hali ikawa tofauti kutokana na ukoo wa Mligula kuporomosha matusi na vitisho kwa Bwana Mwaigaga,ambaye alitoa taarifa Polisi na kufunguliwa kesi mbili dhidi ya ukoo huo,ambapo kesi ya kwanza yenye nambari MB/IR/57/67/2012  ya kutishia kuua kupitia njia ya mtandao na kesi ya pili ya Jinai 551/2012 ya kutoa kashifa mbele ya umma na kupora mali za marehemu.

Mnamo Julai 19,mwaka huu Katibu wa mila wa kabila la Kisafwa Chifu Mwalwego alipokea ombi la msamaha kutoka kwa familia ya Mligula kuomba wapatanishwe na ukoo wa Mwaigaga,baada ya kugundua wamefanya makosa ya kuchukua mali za marehemu badala ya kuziacha katika nyumba hiyo ambapo marehemu wameacha watoto watatu wawili wa kiume na mmoja wa kike ambao walipaswa kuacha mali hizo.

 Baada ya kupokea ombi hilo Chifu huyo aliwasiliana na Bwana Mwaigaga ambaye alikubali kusamehe na kutaka akutanishwe na ukoo huo Julai 21 mwaka huu majira ya saa nne katika eneo la nyumba ya marehemu iliyopo mtaa wa Utukuyu na kwamba yeye hataki kulipwa fidia yoyote licha ya kudharirishwa lakini ameutaka ukoo huo uchangie maendeleo katika shule tatu za msingi zinazozunguka eneo hilo ambazo ni Shule ya Msingi Itewe ipewe mabati 19 ya gauge 30 na shilingi 100,000 kwa Chifu wa mtaa huo.

Ameongeza kuwa Shule ya Msingi Pankumbi ipewe mabati 19 na shilingi 100,000 kwa chifu wa eneo hilo na Shule ya msingi Mwashoma ipewe mabati 19 na  shilingi 100,000 na Chifu Mwanshinga apewe shilingi 200,000 kama msuluhishi wa mgogoro huo.

Hata hivyo Julai 21 mwaka huu ukoo wa Mligula,ulilipa shilingi 500,000 na mabati 57 mbele ya uongozi wa Machifu na uongozi wa Kata ya Uyole baada ya kukutanishwa na ukoo wa Mwaigaga.

Kwa upande wake Bwana Allan Mwaigaga alisema hana kinyongo na kuahidi kufuta kesi mahakamani lakini pande zote mbili za familia zishirikiane kuwalea watoto hao walioachwa na marehemu,pia mali zituzwe na nyumba ipangishwe ili pesa zitumike kwa ajili ya kuwasomesha watoto kwani kwa kufanya hivyo iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia za kuhodhi mali za marehemu na kuacha watoto wakihangaika.

TUKIO LA WANAFAMILIA KUGOMBANIA MALI ZA MAREHEMU.

Kamanga na Matukio | 01:32 | 0 comments
Sehemu ya samani iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga,iliyogombaniwa na ndugu zikiwa zimetolewa nje kwa lengo la kuhamishwa katika Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya.
 Baba Mzazi na Kaka wa marehemu Eva wakiwa nje ya nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na  marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga katika Mtaa huo nayo iliingizwa katika mgogoro wa kugombaniwa,hali iliyopelekea Serikali kuingilia kati..
 Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia tukio la kutolewa kwa vyombo vya marehemu vilivyokuwa vikigombaniwa na wanandugu.
 Mama mzazi wa marehemu Eva,anayefahamika kwa jina la Bi. Magreth Mzegeza(70) aliyevalia nguo nyeupe akiwa na baadhi ya waombolezaji.
 Moja ya magari yaliyotumika kuhamishia shehena ya mali za marehemu.
Sehemu ya Sebule ikiwa tupu baada ya vyombo vyote kubebwa na Kijana huyu alikuwa mstari wa mbele katika kuvitoa vyombo vya marehemu.(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya).

HII NI HALI HALISI YA ELIMU YA TANZANIA

Kamanga na Matukio | 02:42 | 0 comments
 Mwanafunzi wa darasa la 5 akigalagala chini ya sakafu kutokana na mwalimu kutokuwepo darasani ni katika Shule ya Msingi Iyovyo,Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
 Mandhari ya moja ya Chumba cha darasa katika Shule ya Iyovyo.
 Wazazi wa Kijiji cha Iyovyo wakiwa katika malumbano juu ya suala la michango kufunjwa na Uongozi wa kijiji hivho. Pichani ni chumba cha darasa kikiwa kimejaa vumbi na baadhi ya wanafunzi kukaa chini.
 Katika kuinua soka kwa watoto walio na umri mdogo,suala la Chandimu huhusika zaidi kutokana na kutengenezwa pasipo gharama yoyote. Tazama pichani wanafunzi wameweka mpira juu ya dawati,huku mwalimu akiendelea kufundisha.
 Utumikishwaji wa wanafunzi katika kazi ngumu kama ubebaji tofari,kuchota maji,kuzagaa kuni nk, bado ni tete kufuatia wanafunzi wa wilayani Chunya kutumikishwa katika kazi hizo.
Mwanafunzi akiwa ametoka mtoni kuteka maji ya mwalimu.
Hii ni moja kati ya adhabu ambayo kwa wanafunzi imekuwa sugu kutokana na baadhi ya walimu wasiokuwa na utu kuwaadhibu pasipo kujali maumivu wayapatayo wanafunzi.(Picha na Ezekiel Kamanga, Chunya)

UHABA WA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI,SERIKALI YASHAURIWA KUANDAA MIKAKATI ENDELEVU JUU YA VIJANA

Kamanga na Matukio | 02:40 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Mbeya
Serikali imeshauriwa kuwa na mikakati maalumu ya kuwaandaa Vijana katika misingi ya kuyapenda masomo ya Sayansi kwa lengo la kuwa walimu watakaobobea katika ufundishaji wa masomo hayo yatakayowasaidia wanafunzi kujitegemea na siyo kutegemea ajira.

Wito huo umetolewa na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari mkoani Mbeya wakati wa mahojiano maalum kuhusiana na uhaba wa walimu wa sayansi mashuleni na kitu ambacho kinapelekea kukosa walimu wa masomo hayo.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Shule ya sekondari Regco iliyopo Jijini Mbeya,Joshua Mwakitalima amesema kuwa ili kujenga kizazi ambacho kitaweza kujitegemea na kupambana na maisha ni vema Serikali ikajikita zaidi katika kuzalisha walimu vijana ambao pia watafundishwa mbinu za kuwawezesha wanafunzi pindi watakapohitimu wajue jinsi ya kujitegemea.

Ameongeza kuwa katika masomo yafundishwayo mashuleni, ni masomo ya Sayansi pekee ndiyo yanaweza kumjengea msingi wa kujitegemea mwanafunzi pindi amalizapo masomo yake bila kutegemea ajira.
  
Aidha ameongeza kuwa hivi sasa Serikali ni kama inaelekea kuua masomo ya sayansi kwa sababu wahitimu wengi ni masomo ya Art na kufanya idadi kubwa ya walimu mashuleni kuwa wa masomo hayo tofauti na walimu wa Sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Juma Iddi ambaye ndiye mwajiri mkuu wa Halmashauri ya Jiji alipohojiwa kuhusu tatizo hilo alikiri kuwepo na kuongeza kuwa hilo ni janga la kitaifa.

Iddi amesema upungufu wa walimu wa sayansi limechangiwa sana na ongezeko la shule nyingi za kata hivyo serikali imeshindwa kuendana na kasi hiyo katika kuleta walimu wa sayansi ambao hata vyuoni ni wachache.

Ameongeza kuwa Jiji la Mbeya linahitaji jumla ya walimu 412 kwa shule zote lakini badala yake kuna walimu 215 hivyo kuwa na upungufu wa walimu 197 ambapo amesema ni upungufu mkubwa na tatizo hilo linatakiwa lipewe kipaumbele.

Aliongeza kuwa tatizo lingine linalosababisha upungufu wa walimu wa sayansi ni kuwahamisha baadhi ya walimu wenye digrii kuwapeleka katika shule zingine ili hali wenye diploma ni wachache na hawajitoshelezi.

Ametanabaisha kuwa Halmashauri ya Jiji ina mpango wa kuongeza walimu wa sayansi katika Mwaka wa fedha wa Mwaka 2012-2013 ambapo katika bajeti yao wanatarajia kupata walimu 86 ambao pia hawataziba pengo la upungufu huo kwa kuwa bado kuna shule zinaongezeka.

WIZI WA MTOTO WA MIEZI 9 NA WIKI MIWILI.

Kamanga na Matukio | 02:39 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Mbeya
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamtafuta mtu aliyehusika na kitendo cha kumwiba mtoto mwenye umri wa miezi miwili katika Kijiji cha Manga Madibira Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo Julai 18 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.

Amemtaja mama wa mtoto huyo kuwa ni Bi.Tabu Chapunga(18),mkazi wa mkunywa na aliibiwa mtoto wake aitwaye Gulo Manga wakati mama yake akiwa amekwenda kuchota maji.

Aidha,amesema kuwa mtu huyo aliingia chumbani kwa mama huyo na kumchukua kichanga hicho na kutokomea nacho kusiko julikana.

Hata hivyo Kamanda Diwani ametoa mwito kwa mtu yeyote mwenye taarifa juu ya mhusika wa tukio hilo ili kuweza kumbaini mtuhumiwa huyo na kufikishwa katika vyombo vya dola.

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA.

Kamanga na Matukio | 05:17 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti Mkoani Mbeya,likiwemo la fundi seremala Furaha Msongole kudondoka juu ya paa la nyumba Mtaa wa Mwenge,Kata ya Vwawa Wilaya ya Mbozi.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Julai 17 mwaka huu,fundi huyo ambaye alidondoka wakati akipaua nyumba ya Mtumishi wa Halmashuri ya wilaya hiyo Bwana Moses Kibona.

Aidha,jitihada za kujaribu kuokoa uhai wake ziligonga mwamba baada ya kufikishwa katika Hospitali ya wilaya hiyo na kugundulika kuwa ameshafariki dunia.

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Michael Mwaipwisi,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tuio hilo.

Tukio la pili limetokea Mji mdogo wa Tunduma,Wilaya mpya ya Momba ambapo mtu au watu wasiofahamika walimpiga hadi kumuua Izzu Simkoko(25),mkazi wa Chapwa,Kitongoji cha Igawa Tunduma.

Mnamo Julai 17 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku mtu huyo anayesadikika kuwa ni mgonjwa wa akili alipopita eneo la Muungano Mwaka Tunduma,aliwakuta akina mama wakipika chakula na kupiga kelele za mwizi,kisha wakazi wa eneo hilo kuanza kumpiga mpaka kumsababishia kifo.

Mwili wake umehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha mji huo huku Polisi wakiendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo la kikatili.

Tukio la mwisho limetokea wilayani humo humo katika Kitongoji cha Luwemba,Kijiji cha Ikonya,Kata ya Bara lililohusisha ukuta wa nyumba kuanguka na kusababisha kifo cha mtoto wa kiume Hekima Sikitu Balanga(3) na kuwajeruhi wazazi wake.

Wazazi wa mtoto huyo aliyefariki ni Bwana Sikitu Balanga(35) na mkewe Roina Jeremiah ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mbozi Mission baada ya kujeruhiwa.

Hata hivyo Diwani wa Kata ya Bara Mheshimiwa Wiston Songa,amewataka wananchi kuamini hiyo ni ajali ya kawaida kutokana na uvumi kuenea kijijini hapo ya kudai kuwa tukio hilo limesababishwa na imani za kishirikina.

Wakati huo huo mazishi ya mtoto Hekima yamefanyika katika kijiji hicho,Mola azilaze roho za marehemu wote watatu mahali pema peponi.

MAAJABU:- KIJANA AFUMANIWA AKIMBAKA NG'OMBE WA JIRANI YAKE ZIZINI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:11 | 0 comments
Na Bosco Nyambege,Rungwe.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Tumsifu Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng’ombe.

Tukio hilo la ajabu yake limetokea Julai 15 mwaka huu majira ya saa mbili za usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya Bwana Leonard Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka   ng’ombe huyo hali iliyopelekea ng’ombe huyo kuanza kupiga kelele kwa kuomba msaada. 

Ndipo wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mara baada ya kuvunja amri ya sita ya kuzini na ng’ombe huyo.

Aidha,kufuatia hali hiyo Kijana Mwambusi aliomba msamaha kwa kitendo hicho lakini wananchi hao hawakujali na mara akajikuta akimwagiwa maji ya baridi na kipigo kikiwa kinaendelea na kusababishiwa maumivu sehemu mbalimbali ya  mwili wake.

Hata hivyo wazazi wa kijana huyo walijaribu kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa wananchi hao ili waweze kumwachia kijana wao kufuatia kipigo alichokuwa akipewa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Andongwisye Mwakalinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewasihi wananchi hususani vijana kumwomba mungu muda wote ili kuondokana na majaribu yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.

COCACOLA YAZIDI KUMWAGA MAMILIONI KWA WATEJA WAKE.

Kamanga na Matukio | 03:21 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Idadi ya washindi wa promosheni ya Vuna Mkwanja inayoendeshwa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya, imeendelea uongezeka mkoani Mbeya baada ya watu wawili kuzawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mwingine shilingi laki moja walizojishindia baada ya kunywa soda za kampuni hiyo.

Washindi hao wamekabidhiwa fedha zao juzi kwenye kituo cha mabasi madogo maarufu kama daladala katika eneo la Sido mbele ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Nafed Sanga, makazi wa Tunduma wilayani Mbozi na Juma Aron Kaseka mkazi wa mji mdogo wa Mbalizi ndio walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja kila mmoja .

Mwingine ni msichana Liliani Jubel ambaye ameambulia shilingi 100,000 baada ya kunywa soda ya Coca Cola kwenye eneo la tukio na kubahatika kushinda kiwango hicho cha fedha.

Wakizungumzia namna walivyofanikiwa kupata zawadi hizo washindi hao wamesema suala ni kunywa vinyaji vinavyozalishwa na kampuni ya coca cola.

Akikabidhi fedha hizo kwa washindi, Meneja Mauzo wa kampuni ya Coca Cola Nyanda za Juu Kusini, William Nguji amesema kuwa ni rahisi kwa mtu yeyote anayekunywa bidhaa za kampuni ya Coca Cola kuibuka mshindi kwani zawadi zilizotengwa kwa ajili ya promosheni hiyo ni nyingi.

Amesema katika promosheni hiyo kuna zawadi ya soda ya bure, fulana, kofia, fedha taslimu shilingi 2,000 na shilingi 10,000 ambazo washindi hukabidhiwa pale pale kwa muuzaji wa vinywaji vya kampuni ya Coca Cola.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger