Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Uuguzi cha Aggrey Jijini Mbeya.
Na Venance Matinya, Mbeya.
Wanafunzi
wanaosoma Chuo cha Uuguzi cha Aggrey kilichopo Sido Mwanjelwa Jijini Mbeya
wameulalamikia uongozi wa Chuo hicho kwa kutosikiliza kero zao pamoja na
kutotoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali.
Wakizungumza
na
waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wanaosomea fani
za
madawa(Clinical Medicine), meno (Dental), Maabara(Laboratory) na
uuguzi(nursing) walisema baadhi ya kero ambazo hazitolewi majibu ya
kueleweka ni
pamoja na kusajili baadhi ya wanafunzi wasiokuwa na sifa.
Walisema
baadhi ya wanafunzi waliosajiliwa katika chuo hicho ni ambao wana alama moja ya
D ya ufaulu katika somo la Baiolojia katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
nne wa taifa hali inayozua wasiwasi juu
ya uwezo wa Wauguzi watakatolewa Chuoni hapo bila kuzingatia ufaulu wa
masomo mengine kama Kemia na Fizikia.
Waliongeza
kuwa mbali na hilo pia Chuo hicho hakina usaji wa kueleweka ambapo wao
wanaoneshwa namba mbili ambazo zinasomoka 116 na 117 ambazo zimetolewa na
Msajili wa Vyuo(Nacte) hali ambayo wanadai kuwa itawasumbua katika mitihani yao
ya mwisho.
Wanafunzi
hao wa Mwaka wa Pili wapatao 120 walienda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata wanapoenda kwenye mafunzo ya
Vitendo(Field) hupewa kazi ambazo hawajawahi kuzisoma katika mtaala hivyo
kubaki wababaishaji na watazamaji tu bila kujua namna ya kufanya ambapo pia
walidai kuwa hata wakiwa kwenye mazoezi hayo hakuna Mwalimu anayepita
kufuatilia mwenendo wake.
Walisema
katika utaratibu wa kufanya mazoezi ya vitendo wanafunzi walipaswa kupewa fedha
za kujikimu ambazo ni Shilingi 150,000/= kwa kila mtu lakini tangu waanze Chuo
hicho hawajawahi kupewa fedha hizo ambapo wakidai kwenye uongozi wanashindwa
kupewa majibu ya kueleweka.
Kutokana
na madai hayo wanafunzi hao wamejaribu kufanya mgomo na maandamano takribani
mara mbili ili kushinikiza uongozi kuwapatia majibu ya kueleweka lakini juhudi
zao zimekuwa zikigonga ukuta kutokana na jeshi la Polisi kuwahi eneo la tukio
na kutuliza jitihada zao na kuendelea kutoa ahadi kuwa watarekebisha.
Februari
28, Mwaka huu, wanachuo hao walijaribu kufanya maandamano kushinikiza uongozi
wa Chuo hicho kutolea ufafanuzi madai yote ya wanachuo ambapo uongozi huo
uliwaahidi kurekebisha matatizo yote yaliyojitokeza lakini hali hiyo
haikufanyika hadi yalipotokea maandamano mengine yaliyozimwa na jeshi la
polisi.
Katika
maandamano ya hivi karibuni wanafunzi hao walikuja na hoja mpya ambayo walidai
kuwa tangu wanafunzi wa mwaka wa kwanza waanze masomo hawajapelekwa kwenye
mafunzo ya vitendo kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati ilitakiwa kabla yakufunga
mwaka wawe wamesoma.
Akijibu
tuhuma hizo Meneja wa Chuo hicho Kamugisha alisema Suala la usajili kuwa namba
mbili linatokana na Wizara kutoangalia vizuri mtiririko wa usajili ambapo
walitoa namba ya mbele na baadaye kujikuta namba moja imerukwa ambayo ni 117
badala ya 116 hivyo kusababisha utata huo.
Alisema
kutokana na hilo waliamua kulifuatilia ambapo Wizara yenyewe ilibaini kufanya makosa ambapo
waliamua kuiondoa namba 117 na kuitaka Aggrey kutumia namba 116 ambayo
hawajaifuta katika baadhi ya matangazo yao na kuongeza kuwa katika kuwaridhisha
wanafunzi waliamua kutuma wanafunzi Wizarani ambao walileta majibu kwa wenzao.
Kuhusu
kusajili wanafunzi wasio na sifa bado Meneja huyo alisema tatizo liko Wizarani ambao wamekuwa wakibadilisha mitaala
kila mara ambapo mara ya kwanza walitoa sifa kuwa anayetakiwa kujiunga na
masomo ya uuguzi ni lazima awe na ufaulu wa alama ya D katika Somo la
Baiolojia.
Aliongeza
kuwa mtindo huo umekuwa ukileta
sintofahamu kwa wanafunzi ambao hawajaambiwa utaratibu huo hivyo kusababisha
kudai maelezo ambayo baada ya kuambiwa wamekuwa wakisahau na kujikuta
wakiendelea kuibua matatizo mengine.
Alienda
mbali zaidi kuwa chanzo cha migogoro hiyo ni kutokana na baadhi ya wakufunzi
kutuhumiwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi hali iliyosababisha uongozi wa
Chuo kuwafukuza kazi jambo ambalo lilileta mvurugano chuoni hapo.
Aliongeza
kuwa baada ya kutokea hali hiyo uongozi wa chuo ulilazimika kuwarudisha
Wakufunzi hao kuendelea kufundisha licha ya kuonesha utovu wa nidhamu
kazini ambapo uongozi wa chuo umeshindwa
kuchukua hatua yoyote.
Hata
hivyo kufuatia uwepo wa kashfa hizo chuoni hapo baadhi ya wananchi na wadau wa
Elimu wameitupia lawama chuo hicho kwa madai kuwa wanazalisha wauguzi wasiokuwa
na sifa huku wakitolea mfano kwa sakata la daktari aliyewahi kumfanyia upasuaji
wa Kichwa badala ya mguu.
Waliiomba
Serikali kuingilia kati utaratibu wa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kukagua sifa
za wanafunzi waliojiunga na chuo hicho na wakufunzi waliopo hapo kama wanastahili
kuendelea na kazi au kusimamishwa.
Walisema
wanachojaribu kukitengeneza ni hatari kwa taifa na vizazi vijavyo kutokana na
hatua wanazoenda nazo ambapo wanafunzi wanashindwa kufanya mazoezi ya vitendo
na wakienda kufanya mazoezi hayo hushindwa kuendana na mazoezi kwa kile
wanachodai kutofundishwa darasani.
Hata
hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa wanafunzi hao wanalipa
ada ya Shilingi Milioni 1 na Laki mbili (1,200,000/=) kwa mwaka kiwango ambacho
ni kikubwa kulingana na hali ya uchumi wa Watanzania wengi ilivyo sasa.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo hicho Neema Mwambusi alipopigiwa kuhusiana na tuhuma
za chuo hicho aliishia kujibu kuwa matatizo hayo yapo lakini yanapaswa
kumalizwa kiubinadamu bila ya kuhofia uchumi wa wazazi na kizazi kinachozalishwa kutokana na elimu
inayotolewa chuoni hapo.