Hawa Mathias,Mbeya.
Jeshi
la
polisi Mkoani Mbeya linawashikiliwa watu wawili akiwemo mwanamke
wakazi wa kijiji cha Madibila na Mkunywa Wilayani mbarali kwa tuhuma
za kupatika
na silaha pamoja na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Akitoa
taarifa
kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Athuman
Diwani
alisema kuwa watuhumiwa hao walikamtwa kwa nyakati tofauti na askari wa
wanayamapori (TANAPA) na akari wa jeshi la polisi walipokuwa katika
doria za kusaka waharifu
Alisema kuwa katika tukio la kwanza Christian Mhangole (40) mkulima alikamatwa na polisi akiwa na
siraha aina ya SMG yenye namba
88560 ikiwa na risasi 50 ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko maarufu
kama( sulphet ).
Diwani alisema kuwa mara baada ya
uchunguzi zaidi mtuhumiwa huyo alibainika kuwa na nyara za serikali ikiwa ni
pamoja na nyama ya nyati kilo 15 ,nyama ya tembo kili 17 ambazo zilikuwa
zimefichwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kwamba siraha aliyokamatwa nayo
imekuwa ikimilikiwa kinyume cha sheria.
Aidha kamanda Diwani alisema mtuhumiwa
baada ya kuhojiwa alikiri kujihusisha na biashara ya uwindaji haramu wa wanyama
pori na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi
kukamiliki kujibu tuhuma zinazomkabili.
Katika tukio la pili mwanamke kijiji cha Mkunywa wilayani mbarali Emaliana Ndemo (30) anashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma za kupatikana na siraha aina ya Reffle yenye namba B 58221
ikiwa imefichwa chumbani ndani ya nyumba
yake .
Diwani alifafanua kuwa kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo kulitokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na jeshi la
polisi na kwamba ilikuwa ikitumiwa na mume wa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina za
moses mlingamolo (30) ambaye alifanikiwa
kukimbia na polisi wanaendelea na msako
ili aweze kufikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.
Aidha kamanda wa polisi ametoa wito kwa
wananchi kuwafichua watu wanaomiliki siraha kinyume cha sheria kwani
wanachangia uvunjifu wa amani kwa wananchi wasiokuwa na hatia na kwamba
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi
kukamilika.
0 comments:
Post a Comment