Pages


Home » » SERIKALI YAOMBWA KUANGALIA UPYA SUALA LA UPANUZI WA HIFADHI YA WANYAMA

SERIKALI YAOMBWA KUANGALIA UPYA SUALA LA UPANUZI WA HIFADHI YA WANYAMA

Kamanga na Matukio | 05:59 | 0 comments
Na Esther Macha, Mbarali 
Baadhi ya wananchi waliohamishwa na serikali kupisha upanuzi wa Hifadhi ya Wanyama ya Ruaha wilayani Mbarali Mkoani Mbeya waliiomba serikali kuangalia upya suala hilo la kuzidi kupanua maeneo  kwa ajili ya  wanyama kuliko binadamu kwani hadi sasa Tanapa inataka kuwahamisha wakazi hata wa vijiji jirani na hifadhi hiyo jambo ambalo walidai kuwa hawatakuwa tayari kuvumilia hali hiyo ya kunyanyaswa kwaajili wanyama.

Wamesema kuwa kitendo hicho kimewaongezea umasikini kwa kuwa hivi sasa wanaishi maisha ya kuganga njaa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wakati mwandishi wa mtandao huu alipotembelea maeneo walikohamishiwa na kujionea maisha duni wanayoishi kama wakimbizi huku wakiwa hawana maeneo mazuri kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.


Walisema kuwa tangu waondolewe katika maeneo yao ambayo waliyatumia kuendesha shughuli zao za kila siku ikiwemo  makazi ya kudumu, wamepelekwa kwenye maeneo ambayo hayakidhi matakwa yao na maisha yao yamekuwa ya kuganga njaa muda wote  hali inayosababisha umaskini wao kuongezeka mara dufu.


Mmoja wa wananchi hao ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mapogolo, kata ya Miombweni, Shimba Nega alisema kuwa Hifadhi hiyo imewapelekea wananchi kuwa katika maisha magumu huku maeneo waliondolewa wanashangaa kuona hayafanyiwi kazi yoyote na imebaki kuwa pori lisilo kuwa na kazi muhimu.


Mkazi huyo ambaye ni miongoni mwa waliohamishwa na Tanapa toka kijiji chao  cha awali cha Ikoga alieleza kuwa hali hiyo imewafanya kupoteza mwelekeo kabisa wa maisha yao huku wakijikuta wanashindwa hata kulea familia yao kwa vile tegemeo lao kubwa ni ardhi waliokuwa wakiitumia kwa ajili ya kilimo ili wapate kuwatunza watoto wao kuchukuliwa na Tanapa.


“Hivi sasa tumekuwa masikini wakutupwa na serikali tangu ituhamishe maeneo yetu tuliokuwa tumejiwekea misingi ya maisha imetusahau na kukutupa kabisa” alisema .


“Hapa unavyoniona nina watoto 38 wa kuzaa mimi mwenyewe na sina kitu chochote na mifugo yangu yote nimeuza ili nipate kulisha familia yangu , na kwamba kipindi cha nyuma kabla serikali haijatuhamisha nilikuwa najivunia ardhi kwa ajili ya kilimo na watoto wangu nilikuwa nawapeleka shambani kulima hivyo sikuwa na shida yoyote kuhusu chakula na mahitaji mengine ya watoto hawa lakini sasa hali imekuwa ngumu sana” alisema mzee Nega.


Akuzungumza na gazetui hili kwa njia ya simu akiwa Jijini Dar es Salaam Mbunge wa Jimbo la Mbarali Bw. Modestus Kirufi alise kweli hali hiyo ipo kwa wananchi na kuongeza kkuwa mara nyingi maeneo ambayo ni mapya kawaida wananchi wanakuwa na maisha magumu.


Hata hivyo aliiomba serikali inapohamisha wananchi wake ijaribu kuangalia hali halisi ya mazingira wakati wanawapeleka wananchi katika maeneo mapya kutokana na kutokuwa na miundo mbinu mizuri.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger