Pages


Home » » WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAJIPANGA KUKABILIANA NA HALI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI.

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAJIPANGA KUKABILIANA NA HALI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI.

Kamanga na Matukio | 02:18 | 0 comments
Hawa Mathias,Mbeya.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imejipanga na kuweka mikakati  kushirikiana na wadau mbalimbali  ili kukabiliana na hali ya usafi wa mazingira  nchini na kuhakikisha jamii inatumia vyoo safi na salama  na kuondokana na adha ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi msaidizi,afisa afya mkuu Tanzania  wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Elias Chinamo katika maadhimisho ya siku ya choo duniani yaliyofanyika  wilayani rungwe Mkoani Mbeya.


Alisema kuwa ili kufikia malengo ya mileniam ya utunzaji wa usafi wa mazingira jamii inatakiwa kuwa na mwamko wa kujikita katika kutunza hali ya mazingira  na kujenga vyoo bora ili kuondokana na adha ya kusambaa kwa vinyesi  vinavyochangia  kusababisha magonjwa ya milipuko na kuhara.


Aidha alisema kuwa  katika kufanikisha maadhimisho hayo na tumeweka mikakati ya  kufikisha  ujumbe kwa wananchi   kwa kutoa elimu ya usafi wazingira na matumizi ya vyoo bora  kupitia vipeperushi ,na vyombo vya habari.


"Pia tumeandaa mashindano ya usafi wa mazingira  katika shule za msingi na sekondari ,kata na kaya,na taasisi mbalimbali binafsi na serikalini"Alisema.

Chinamo alifafanua kuwa hali ya usasi wa mazingira ya vyoo bora bado  ni changamoto kubwa nchini na kwamba jitihada za pekee za hitajika  kwani takwimu zinaonyesha   asilimia 12 pekee ya kaya nchini ndizo zenye vyoo bora na salama kwa afya za watumiaji.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger