Pages


Home » » TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14 /11/2012.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14 /11/2012.

Kamanga na Matukio | 03:34 | 0 comments
WILAYA YA MOMBA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 13/11/2012 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA UHAMIAJI WALIWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 25 KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI WAKIWA WAMEHIFADHIUWA NYUMBANI KWA MWENYEJI WAO AITWAYE TRIFON S/O TITTO, MKINGA, 20YRS, MFANYABIASHARA  NA MKAZI WA TAZARA TUNDUMA.  WAHAMIAJI HAO WAMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA POLISI TUNDUMA KWA HATUA ZAIDI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA WATU WANAOWATILIA MASHAKA/WAGENI WASIOELEWEKA JUU YA UWEPO WAO KWANI WENGINE HAWANA NIA NJEMA ILI WAKAMATWE NA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA . AIDHA ANATOA ONYO KWA MTU/WATU WENYE TABIA YA KUWASAFIRISHA NA KUWAHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU WAACHE TABIA HIYO MARA MOJA NA ATAKAEBAINIKA ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA  KISHERIA .

WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 13/11/2012 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KITONGOJI CHA MADIZINI KIJIJI CHA MALEZI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SALUM S/O MASANJA, 19 YRS, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MADIZINI AKIWA NA BHANGI  KETE KUMI TA TANO [15] SAWA NA GRAMU 75 . AKIWA AMEIFICHA KATIKA MFUKO WA KHAKI. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI  PIA NI KINYUME CHA SHERIA.

WILAYA YA MBEYA MJINI – MWANAMKE MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
MNAMO TAREHE 12/11/2012 MAJIRA YA SAA 10:30 HRS HUKO KATIKA MTAA WA MAJENGO KASKAZINI JIJINI MBEYA. WILVINA D/O LENATUS MKANDALA, MIAKA 24, MHAYA, MKAZI WA MAJENGO, MAMA WA NYUMBANI ALIKAMATWA KWA KOSA LA KUMNYANYASA KIJINSIA MTOTO WA DADA YAKE AMBAYE ALIKUWA AKIMLEA AITWAYE ANETH D/O GASTO, MIAKA 5, MHAYA, KWA KUMFUNGIA NDANI YA NYUMBA, KUMCHOMA KWA MOTO SEHEMU YA MKONO JUU YA KIWIKO CHA MKONO WA KUSHOTO NA KIGANJA, KUMNYIMA CHAKULA NA KUMPIGA MARA KWA MARA KWANI MTOTO HUYO AMEKUTWA NA MAKOVU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. MTUHUMIWA AMEKIRI KUYATENDA MAKOSA HAYO YA UNYANYASAJI. MHANGA AMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU NA HIFADHI WAKATI TARATIBU ZA KUWASILIANA NA WAZAZI WAKE HALISI WALIOKO MKOANI KAGERA WILAYA YA MULEBA ZINAFANYIKA . MTUHUMIWA YUKO MAHABUSU KWAAJILI YA USALAMA WAKE NA HATUA ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII HUSUSANI WAZAZI/WALEZI KUACHA TABIA YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WATOTO WADOGO KWANI NI KINYUME CHA SHERIA/ MAADILI PIA NI KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WANAOKUWA NA TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOFANYA MATENDO HAYA YA KIKATILI KUZITOA TAARIFA HIZO KWENYE MAMLAKA HUSIKA KWA SIRI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE LIKIWEMO JESHI LA POLISI AMBALO LINA KITENGO CHA KUSHUGHULIKIA MAKOSA YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA  [TPF NET – MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANI]

WILAYA YA RUNGWE – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 13/11/2012 MAJIRA YA SAA 16:30 HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA BUGOBA KIJIJI CHA BUGOBA KILICHOPO  MTAA WA KISONDELA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WALIWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 21 RAIA WA ETHIOPIA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA BUGOBA. WAHAMIAJI HAO WALIKUWA WAMEJIFICHA KATIKA KICHAKA KILICHOPO KITONGOJI CHA BUGOBA .TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAANDALIWA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA WATU WANAOWATILIA MASHAKA/WAGENI WASIOELEWEKA JUU YA UWEPO WAO KWANI WENGINE HAWANA NIA NJEMA NA NCHI YETU.

Signed By,
     [ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger