Na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watoto
watatu wa familia moja wameteketea kwa moto uliotokea majira ya saa 2
na dakika 15 usiku Novemba 7 mwaka huu, katika Kitongoji cha Buswema,
Kijiji cha Ilundo, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Baba
mzazi wa watoto hao Nuru Sambo(31), amewataja watoto hao walioteketea
kwa moto kuwa ni pamoja na George Nuru(9), Mevis Nuru(4) na Winnie
Nuru(2) wote kwa pamoja walikuwa wamelala chumbani wakati mama yao mzazi
Bi. Sifa Asagwile(27), alikuwa amekwenda kumchukua mtoto mwingine
Dontisia Nuru(6) aliyekuwa kwa Bibi yake aitwaye Kipesile.
Baba
wa watoto hao amesema kuwa wakati wa tukio yeye na mkewe walikuwa
hawapo na alipokuwa anarejea nyumbani alikutana na kundi la watu
waliokuwa wakielekea nyumbani kwake na wengine kumpa pole asijue
kilichotokea na alipofika nyumbani alikuta alikuta nyumba ikiteketea na
wanawe wakiwemo ndani ambapo walifariki papo hapo.
Nyumba
hiyo ilikuwa imeezekwa kwa nyasi na mpaka sasa chanzo cha moto huo
hakijaweza kufahamika, ingawa kuna tetesi kuwa huenda moto huo
ulisababushwa na kiberiti kilichowashwa kabla ya watoto hao kulala.
Aidha,
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilundo Bwana Jairo Mpakama amethibitisha
kutokea kwa vifo hivyo na kwamba mazishi ya watoto hao yatafanyika
Novemba 8 mwaka huu, majira ya saa 8 mchana na kuhudhuriwa na wananchi
kutoka vijiji mbalimbali waliokuja kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Tukio
jingine Meck Laiton Mbegesi(34) mkulima na mkazi wa Kitongoji cha
Utyegu Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, mkoani hapa ameuawa na mtu au watu
wasiofahamika kwa kukatwakatwa na mapanga maeneo mbalimbali ya mwili
wake.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Viwandani, Kijiji cha Matelemehe Bwana Fidelis Dominicus
Pelela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mazishi
yamefanyika Novemba a7 mwaka huu kijijini hapo baada ya uchunguzi wa
Daktari/.
Mdogo
wa marehemu Bwana Emmanuel Manyuki Laiton(28), amesema marehemu
alirejea nyumbani usiku majira ya saa tatu usiku Novemba 6 mwaka huu
baada ya kutoka katika biashara zake eneo la kilaabuni na baadae
aligongewa mlango na watu waliofika hapo kwa kutumia pikipiki kisha
kumchukua marehemu mita kadhaa kutoka nyumbani hapo kisha kumpiga
mapanga kichwani, masikioni na mdomoni ambapo alivuja damu nyingi na
kusababisha kifo chake papo hapo.
Hata
hivyo mwili wa marehemu ulikutwa mita kadhaa kutoka nyumbani ambapo
ulitambuliwa na wapita njia na kutolewa taarifa Ofisi ya Kijiji na
kisha kutambuliwa na mdogo wa marehemu Bwana Laiton, ambapo taarifa
polisi ambao walifika eneo la tukio na kuuanza uchunguzi kuhusiana na
tukio hili.
Baadhi
ya wananchi wamedai kuwa tukio hilo huenda likahusishwa na ulipizaji
kisasi kwani uhai wake marehemu alikuwa akijihusisha na vitendo vya wizi
na kusababisha kero kijijini hapa.
0 comments:
Post a Comment