Miili ya watoto Timotheo Omary(5) na Thadeo Bryston Malila(5) waliofariki kupitia ajali iliyotokea Kijiji cha Imezu,Kata ya Inyala Mkoani Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dk. Norman Sigalla akiwa na Meneja wa TANROADS mkoani Mbeya wakibadilishana mawazo namna ya kuweka matuta eneo la Imezu lililokithiri kwa ajali.
Baadhi ya wananchi wa Imezu wakisukuma gogo kupeleka barabarani kwa ajili ya kufunga barabara kufuatia ajalihiyo.
Mwandishi wa habari Bwana Charles Mwaipopo akiwa eneo la tukio.
Na Ezekeil Kamanga Mbeya
Matukio ya ajali yameendelea kuandamwa Mkoa wa Mbeya baada ya wananchi wa Kijiji cha Imezu kata ya Inyala wilaya ya Mbeya Vijijini jana kulazimika kufunga bara bara ya Mbeya Dar es Salaam kwa masaa sita baada ya kutokea
ajali iliyoua watoto wawili wa chekechea wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka
mitano mpaka sita wanafunzi wa shule ya
msingi Imezu.
Imeelezwa kuwa wananchi hao waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na ahadi za serikali
kupitia wakala wa bara bara ambazo zimekuwa hazitekelezwi katika eneo hilo la la shule ya msingi Imezu na kuendelea kukatiza uhai wa
watu.
Akizungumza na gazeti hili Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha
Imezu Bw. Seif John alisema kuwa tukio la kufungwa kwa bara bara hiyo limetokea
majira ya saa 1.15 asubuhi baada ya watoto hao kugongwa na gari aina ya Lori la mafuta
yenye namba T 698 BVY lenye tela namba T 798 BVA lililokuwa likiendeshwa na dereva Dominick Anton Mwakalundwa(34) likitokea Mbeya
kwenda Mkoani Iringa liligonga watoto
hao waliokuwa pembeni ya bara bara wakitoka shule.
Bw. John alisema kuwa baada ta tukio hilo kutokea wananchi
walijaa eneo la ajali na kuanza
kufunga bara bara kwa kutumia magogo na
mawe ili kuzuia magari yasipite eneo
hilo kwa lengo la kushinikiza serikali kuweka matuta ili kuzuia ajali.
“Unajua haya matukio ya ajali yamekuwa yakitokea mara kwa mara
katika eneo hili la shule ambapo mpaka
sasa zaidi ya watu 30 wameshafariki
dunia kwa ajali kama hizi, sasa hiii hali tumechoka kwani zimekuwa ahadi tu
bila utekelezaji wowote tunashindwa kuelewa kinachofanya wasiweke matuta nini wakati uwezo upo, wanasubiri mpaka madhara makubwa
yatokee zaidi ya hili “alihoji mwananchi huyo.
Hata hivyo baada ya tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt.
Norman Sigalla aliwaomba wananchi kufungua bara bara wakati serikali kwa kushgirikiana na wakala wa bara bara (TAN
ROADS) ikiwa inaweka utaratibu wa kuweka
matuta hayo haraka iwezekanavyo.
“Nimesikia kilio chenu kwani hata mimi msiba huu umenigusa
kwani naliagiza jeshi la polisi mKoani hapa kuwachukulia hatua kali madereva wataoendesha magari kwa mwendo kasi na kwamba watozwe faini na adhabu kali ambayo
itawafanya wawe na nidhamu na askari
wasiwe marafiki wa madereva”alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Aidha wananchi hao
walisema kuwa wamechoshwa na mwendo kasi
wa madereva katika eneo hilo kwani na kuongeza kuwa ajali hizo zimekuwa
zikipoteza nguvu kazi ya Taifa kwa kiasiu kikubwa.
Hata hivyo baada ya tukio hilo kutokea dereva wa gari iliyosabisha ajali hiyo alienda
kujisalimisha mwenye katika kituo kidogo cha Inyala kwa usalama kutokana na wananchi kuwa na
hasira.
Akizungumza katika
eneo la tukio Diwani wa kata ya Inyala Bw. Libareto Mwalingo alisema kuwa
ameandika barua kwa wakala wa bara bara mara
nyingi kuomba kuwekewa matuta
hayo bila mafanikio yeyote huku
matukio hayo yakiendelea kumaliza wananchi wa eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wa enbeo hilo walisema kwamba kama
serikali imeshindwa kuweka matuta basi ihamishe
shule kwani watoto walio wengi wanaosoma shule hiyo wanatoka upande wa
pili wa bara bara ambao unawalazimu
kuvuka bara bara.
Miili ya watoto hao
imepelekwa katika hospitali ya Inyala kwa uchunguzi ili iweze kukabidhiwa kwa ndugu zao kwea
maziko ambapo watoto hao wote ni wa kiume.
Hata hivyo watoto waliofariki wametambuliwa kwa majina ya Timotheo Omary(5) na Thadeo Bryston Malila(5) wote ni wanafunzi wa awali.
0 comments:
Post a Comment