WILAYA YA MBARALI -
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO
TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA 14:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLANGALI BARABARA
YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI DFP 7322 AINA YA NISSAN
PATROL MALI YA BARAZA LA KILIMO DSM LIKIENDESHWA NA DEREVA JACKSON S/O PAUL
LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA IRINGA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE BADO
HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA
25- 30 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MISSION CHIMALA. DEREVA AMEKAMATWA.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA NA TAHADHARI
YA MATUMIZI YA BARABARA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI. AIDHA
ANATOA WITO KWA WAKAZI WA ENEO HILO KUFIKA HOSPITALINI HAPO ILI KUUTAMBUA MWILI
WA MAREHEMU.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO
TAREHE 25.11.2012 MAJIRA YA SAA 21:20HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI – MALEZA
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MWASHI D/O LUGWISHA,MIAKA 25, MSUKUMA,MKULIMA MKAZI WA
SAZA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA NI
MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE HARAMU KWANI NI HATARI
KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.
KUPATIKANA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA
MNAMO
TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA SAA 17:20HRS HUKO MPINDO BULYAGA – TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA WALLACE S/O MSAMATI ,MIAKA 60, MMAKUA ,MKULIMA MKAZI
WA MPINDO BULYAGA AKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1 NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO .
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE HARAMU KWANI NI HATARI
KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment