Polisi katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki ya Kenya wanachunguza mauaji
ya mjumbe mwandamizi wa kamati ya polisi jamii ya Wajir yaliyotokea siku
ya Jumatano (tarehe 16 Novemba).
Issa Aalim, ambaye hayumo katika picha,
alisaidia polisi kufichua dafina ya silaha kwenye Makaburi ya Ahmed
Liban mwezi Oktoba. [Na Bosire Boniface/Sabahi]
Watu wasiojulikana wenye silaha walimpiga risasi Issa Aalim, aliyekuwa
na umri wa miaka 40, ndani ya nyumba yake katika kitongoji cha Halane
mnamo saa 1 jioni kabla ya kukimbia kutoka eneo la tukio, mkuu wa polisi
wa Wajiri James Mutungi aliiambia Sabahi.
"Aalim alipigwa risasi mbili kichwani na moja kifuani," Mutungi alisema. "Alifariki hapo hapo."
"Hatuwaachi al-Shabaab au wafuasi wao katika kuhusika na mauaji haya kwa
sababu marehemu alikuwa na nafasi kubwa katika vita dhidi ya siasa kali
wilayani," alisema. "Wakati huo huo, hatuachi kufikiria sababu
nyingine."
Kamishna wa Jimbo la Wajir Naftali Mungathia alisema kuwa Aalim alikuwa
mjumbe wa Kamati ya Polisi Jamii ya Wajir ambaye aliwasaidia maafisa
katika kushughulikia masuala ya usalama mjini.
0 comments:
Post a Comment