Hawa Mathias,Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya
linawashikilia watu 10 wanaosadikiwa
kuwa ni askari wa jeshi la wananchi (JWTZ) kikosi cha 44 Kj kambi ya mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya
kijana Petro Sanga(25) kwa kumchoma kisu shingoni na mdomoni na wengine sita kujeruhiwa kwa kumshambulia kwa kipigo.
Taaarifa
iliyotolewa katika vyombo vya
habari na Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman zilieleza kuwa
tukio hilo lilitokea novemba 18 majira ya 3.00 za usiku ambapo
marehemu alikuwa akipata kinywaji katika baa ya power night club.
“Awali marehemu alikuwa akipata kinywaji
katika baa hiyo na kwamba walivamia na
kuanza kuwashambuliwa wananchi waliokuwepo akiwemo marehemu ambaye alipingwa sehemu
mbalimbali za mwili wake kwa kutumia mateke,mikanda,marungi,sime na mapanga na kisha kumchoma kisu na kwamba marehemu
alijaribu kujiokoa kwa kukimbilia baa iitwayo vavenemwe “Alisema Diwani.
Awali diwani alisema mara marehemu baada
ya kupoteza fahamu na kukimbizwa katika
hosptali teule ya ifisi iliyopo katika
mji mdogo wa mbarizi alifariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya na kuvuja damu nyingi.
Diwani alisema kuwa uchunguzi umebaini
kuwa chanzo cha vurugu hizo na kushambulia wananchi kwa kipigo na kusababisha
kifo ni kutokana na askari wa jeshi Geodfery
Matete (30) kushambuliwa na walinzi wa
kilabu cha pombe za kienyeji
kilichojulikana kwa jina la (DDC) novemba 17 mwaka huu
.Alisema
kuwa kufuatiwa tukio hilo la kushambuliwa kwa
mwanajeshi lilipelekea jeshi la polisi
kuwashikilia walinzi wanne kwa mahojiano zaidi na aliwataja kuwa ni
Frenk Mtasimwa(25) Mure Julius (26) Omari Charles (28) na Regnad
Mwampete wakazi wa izumbwe mbeya vijijini.
Diwani alisema kuwa majina ya watuhumiwa hao
yatatajwa baadaye kwani bado uchunguzi unaendelea na kwamba ametoa wito kwa
vyombo vya dora kutojichukulia sheria mikononi kwa kufanya vurugu bila kujari
madhara yanayojitokeza hususan kuharibu mali hususan magari kwa kuvunja vioo na
kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Aidha
alisema kuwafutia tukio hilo jeshi la
polisi linafanya jitihada za dhati kwa mujibu wa sheria ili haki itendeke na
kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi pindi
matukio hayo yanapotokea.
0 comments:
Post a Comment