MAHAKAMA ya
hakimu mfawidhi Mkoa wa Mbeya
imeahirisha Kesi inayomkabili mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga Rice
Project lililopo Wilayani Mbarali ya kuharibu mazao ya wakulima kwa sababu ya kukosekana mkalimani
wa lugha ya kiingereza na Kiswahili.
Mwezi February
2012 Serikali ilimfikisha mahakamani mwekezaji huyo katika mahakama ya Wilaya
ya Mbeya kwa makosa mawili ya kula njama na kutenda kosa kuharibu mai za
Wananachi na kusababisha hasara ya zaidi ya shs 800 milioni.
Iidaiwa
mahakamani hapo kuwa mwekezaji huyo alitenda kosa kati ya Januari 12 hadi 14
mwaka huu ambapo alimwaga sumu katika mashamba
hekari 489 .5 ya wananachi zaidi ya 154 wa kijiji cha kapunga kwa kutumia
ndege kunyunyuzia dawa.
Watuhumiwa
wa kesi hiyo ni pamoja na Meneja wa shamba Walder Vermaak,Afisa ugani Serger
Berkker na Rubani wa ndege Andries Daffe wote raia wa Afrika Kusini.
Akiahirisha
kesi hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mkoa Michael Mteite alisema kuwa
kutokana na kukosekana kwa mkalimani wa
lugha Kiswahili na Kiingereza anaihairisha kesi hiyo hadi January 7 hadi 10
mwaka 2013 itakaposiklizwa kwa mfululuzo.
Alisema
katika siku hizo za kesi mashahidi 40 watatoa ushahidi wao ambapo kila siku ya kesi
watasikilizwa mashahidi 10 na kwamba ili haki itendeke ni lazima apatikane
mkalimani.
Awali akieleza
mahakamani hapo mwendesha mashitaka wa Serikali Christina Joas alisema kuwa
upande wa mashitaka unategemea kuleta mashahidi 154 na vielelezo viwili ikiwa
ni pamoja na ramani ya eneo la tukio na taarifa ya halmashauri ya Wilaya ya
Mbarali.
Katika kesi
hiyo Wakili wa utetezi Ladslaus Rwekaza aliioma mahakama kumkabidhi majina ya
mashahidi na vielelezo hatua iliyopingwa na hakimu kwa madai kwamba vielelezo
atapatiwa lakini siyo majina ya mashahidi.
0 comments:
Post a Comment