Pages


TANGAZO LA KIFO CHA MTANGAZAJI WA BOMBA FM CLEMENCE MPEPO

Kamanga na Matukio | 10:51 | 0 comments
 
 TANGAZO: KWA MASIKITIKO MAKUBWA UONGOZI WA REDIO BOMBA FM, TUNATANGAZA KIFO CHA MFANYAKAZI WETU CLEMENCE MPEPO "MZEE WA MAKABILA" ALIYEFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI. KWA TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA JUU YA UTARATIBU WA MAZISHI NA PIA ENDELEA KUSIKILIZA REDIO.

Msanii Wa Bongo Movie John Maganga Azikwa.

Kamanga na Matukio | 01:52 | 0 comments
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salam za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es salaam. Maganga alifariki Jumamosi hii
 Nape (kulia) akiwa kwenye msiba huo
  Msanii wa Bongo Movie,  Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na  Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movie, marehemu  John Maganga
  Wasanii wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam
Nape akizungumza na Rais wa Chama Cha Bongo Movie wakati wa msiba huo

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYAHABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 27/11/2012.

Kamanga na Matukio | 01:51 | 0 comments
WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA 14:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLANGALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI DFP 7322 AINA YA NISSAN PATROL MALI YA BARAZA LA KILIMO DSM LIKIENDESHWA NA DEREVA JACKSON S/O PAUL LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA IRINGA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25- 30 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MISSION CHIMALA. DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA NA TAHADHARI YA MATUMIZI YA BARABARA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA ENEO HILO KUFIKA HOSPITALINI HAPO ILI KUUTAMBUA MWILI WA MAREHEMU.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 25.11.2012 MAJIRA YA SAA 21:20HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI – MALEZA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MWASHI D/O LUGWISHA,MIAKA 25, MSUKUMA,MKULIMA MKAZI WA SAZA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE HARAMU KWANI NI HATARI KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA
MNAMO TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA SAA 17:20HRS HUKO MPINDO BULYAGA – TUKUYU   WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA WALLACE S/O MSAMATI ,MIAKA 60, MMAKUA ,MKULIMA MKAZI WA MPINDO BULYAGA  AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1 NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE  HIYO  . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE HARAMU KWANI NI HATARI KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.

Signed By,
    [DIWANI ATHUMANI – ACP]
                        KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KESI INAYOMKABILI MWEKEZAJI WA SHAMBA LA MPUNGA LA KAPUNGA RICE PROJECT YAAHIRISHWA

Kamanga na Matukio | 01:50 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya
MAHAKAMA ya hakimu mfawidhi  Mkoa  wa Mbeya  imeahirisha  Kesi inayomkabili mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga Rice Project lililopo Wilayani Mbarali ya kuharibu mazao  ya wakulima kwa sababu ya kukosekana mkalimani  wa lugha ya kiingereza  na Kiswahili.
Mwezi February 2012 Serikali ilimfikisha mahakamani mwekezaji huyo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kwa makosa mawili ya kula njama na kutenda kosa kuharibu mai za Wananachi na kusababisha hasara ya zaidi ya shs 800 milioni.
Iidaiwa mahakamani hapo kuwa mwekezaji huyo alitenda kosa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu ambapo alimwaga sumu katika mashamba  hekari 489 .5  ya wananachi  zaidi ya 154 wa kijiji cha kapunga kwa kutumia ndege  kunyunyuzia dawa.
Watuhumiwa wa kesi hiyo ni pamoja na Meneja wa shamba Walder Vermaak,Afisa ugani Serger Berkker na Rubani wa ndege Andries Daffe wote raia wa Afrika Kusini.
Akiahirisha kesi hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mkoa Michael Mteite alisema kuwa kutokana na kukosekana  kwa mkalimani wa lugha Kiswahili na Kiingereza anaihairisha kesi hiyo hadi January 7 hadi 10 mwaka 2013 itakaposiklizwa kwa mfululuzo.
Alisema katika siku hizo za kesi mashahidi 40 watatoa ushahidi wao ambapo kila siku ya kesi watasikilizwa mashahidi 10 na kwamba ili haki itendeke ni lazima apatikane mkalimani.
Awali akieleza mahakamani hapo mwendesha mashitaka wa Serikali Christina Joas alisema kuwa upande wa mashitaka unategemea kuleta mashahidi 154 na vielelezo viwili ikiwa ni pamoja na ramani ya eneo la tukio na taarifa ya halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Katika kesi hiyo Wakili wa utetezi Ladslaus Rwekaza aliioma mahakama kumkabidhi majina ya mashahidi na vielelezo hatua iliyopingwa na hakimu kwa madai kwamba vielelezo atapatiwa lakini siyo majina ya mashahidi.

ASKARI ALIYEFANYA MAPENZI NA MTUHUMIWA WA KIKE KATIKA KITUO CHA POLISI AFUKUZWA KAZINI

Kamanga na Matukio | 01:49 | 0 comments
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
JESHI  la polisi  Mkoani  Mbeya  limefukuza kazi Askari wake Enock Daffa (22)  kwa tuhuma  za kufanya  mapenzi  na mtuhumiwa wa kike  mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha polisi cha mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Kwa mujibu wa  kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  Athuman Diwani   askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba  mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa  anakabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvuliwa na jeshi la polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitopa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za jeshi la polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kuinda maadili ya jeshi la polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo baba mzazi  wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambaco kimetia fedheha familia yake lakini pia kwa jeshi la plisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati  huo  huo  katika  kijiji cha malangali barabara ya Mbeya Iringa Wilaya ya Mbarali gari yenye namba za usajili DFP 7322 aina ya Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisa kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa marehemu bado haujafamika  na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.

KAMANDA WA POLISI ATHIBITISHA:SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA

Kamanga na Matukio | 01:26 | 0 comments

  Kuna habari kuwa msanii  Hussein Ramadhani aliyekuwa maarufu kwa jina la Sharo Millionea, msanii wa muziki na maarufu katika kuwepo kwake katika matangazo kwa style ya aina yake amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari Tanga. 

 Kamanda wa Polisimkoani Tanga, Constatine Masawe amekiri kutokea kwa msiba wa Sharobaro, baada ya kupata ajali katika kijiji cha Lusanga, Muheza ambapo pia ndio nyumbani kwao

R.I.P SHARO MILLIONEA 

 MSIKILIZE KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA  AKIONGEA HAPA

 Alichosema kamanda hiki kama umeshindwa kuisikiliza
 Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
 
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 22/11/2012.

Kamanga na Matukio | 01:52 | 0 comments



WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - MAUAJI
 MNAMO TAREHE 21.11.2012 MAJIRA YA SAA 22:00HRS HUKO KIJIJI CHA MLIWO KATA YA ISUTO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. TAINES D/O KOMBANI,MIAKA 30,MKULIMA,MMALILA,MKAZI WA KIJIJI CHA ISUTO ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE AITWAE YISAMBI S/O CHIKINGA . CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI KWANI MTUHUMIWA ALIKUWA AKIMKATAZA MAREHEMU KUTOTEMBEA OVYO. MTUHUMIWA ALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU AMBAYE ALIKUWA NI MJAMZITO UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA ANATOA RAI KWA JAMII KUTATUA MATATIZO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIKO MTUHUMIWA WAZITOE ILI AKAMATWE.

WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 21.11.2012 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU WANNE RAIA WA ETHIOPIA 1.BARAKA S/O ELIWAU 2.MATHIAS S/O WAKALTO, 3. EFLAUD S/O TEFAKI NA 4.  TAMASKE S/O TADASA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUJIFICHA KATIKA PAGALA. WATUHUMIWA WAPO MAHABUSU TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA SIRI KWA MAMLAKA HUSIKA  DHIDI YA WAHALIFU NA WATU WASIOWAFAHAMU AMBAO WANAWATILIA SHAKA ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Signed By,
    [DIWANI ATHUMANI – ACP]
                                          KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


ASKARI 10 WANAOSADIKIKA KUWA NI ASKARI WA JWTZ KIKOSI CHA 44 KJ WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI.

Kamanga na Matukio | 01:49 | 0 comments
Hawa Mathias,Mbeya.


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia  watu 10 wanaosadikiwa kuwa ni askari wa jeshi la wananchi  (JWTZ) kikosi cha 44 Kj  kambi ya mji mdogo wa Mbalizi  kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana  Petro Sanga(25)  kwa kumchoma kisu shingoni na mdomoni na  wengine sita kujeruhiwa  kwa kumshambulia kwa kipigo.





Taaarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman zilieleza kuwa  tukio hilo lilitokea  novemba 18 majira ya 3.00 za usiku  ambapo marehemu alikuwa akipata kinywaji  katika baa ya power night club.








“Awali marehemu alikuwa akipata kinywaji katika  baa hiyo na kwamba walivamia na kuanza kuwashambuliwa wananchi waliokuwepo  akiwemo marehemu ambaye alipingwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia mateke,mikanda,marungi,sime na mapanga na  kisha kumchoma kisu na kwamba marehemu alijaribu kujiokoa kwa kukimbilia baa iitwayo vavenemwe “Alisema Diwani.








Awali diwani alisema mara marehemu baada ya kupoteza fahamu  na kukimbizwa katika hosptali teule ya ifisi iliyopo  katika mji mdogo wa mbarizi  alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya  na kuvuja damu nyingi.








Diwani alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa chanzo  cha vurugu hizo na  kushambulia wananchi kwa kipigo na kusababisha kifo ni kutokana na  askari wa jeshi Geodfery Matete (30)  kushambuliwa na walinzi wa kilabu cha pombe za kienyeji  kilichojulikana kwa jina la (DDC) novemba 17 mwaka huu





.Alisema kuwa   kufuatiwa tukio hilo la kushambuliwa kwa mwanajeshi  lilipelekea jeshi la polisi kuwashikilia walinzi wanne kwa mahojiano zaidi na aliwataja  kuwa ni Frenk Mtasimwa(25) Mure Julius (26) Omari Charles (28) na Regnad Mwampete wakazi wa izumbwe mbeya vijijini.





Diwani   alisema kuwa majina ya watuhumiwa hao yatatajwa baadaye kwani bado uchunguzi unaendelea na kwamba ametoa wito kwa vyombo vya dora kutojichukulia sheria mikononi kwa kufanya vurugu bila kujari madhara yanayojitokeza hususan kuharibu mali hususan magari kwa kuvunja vioo na kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.








Aidha alisema kuwafutia tukio hilo  jeshi la polisi linafanya jitihada za dhati kwa mujibu wa sheria ili haki itendeke na kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi pindi matukio hayo yanapotokea.

MWANAMKE AIBA SIMU KANISANI, IBADA YASIMAMA KWA MUDA.

Kamanga na Matukio | 01:48 | 0 comments
Stephano Simbeye, Mbozi - Mbeya

Katika hali isiyo ya kawaida Kanisa la Moraviani Usharika wa Tunduma, juzi ilibidi lisitishe kwa muda ibada, baada ya msichana mmoja Tumaini Mbembela (18) ambaye ni mama lishe mjini hapa, kukutwa ameficha simu ya muumini mwenzake katika kitenge cha kumbebea mtoto wa aliyemwibia.

Tukio hilo lilitokea Jumapili katika ibada ya kawaida iliyokuwa ikiongozwa na mchungaji wa kanisa hilo Atumigwe Msokwa,mara baada ya kuwaruhusu waumini wake wafanye toba kufuatia mahubiri yaliyotolewa na Mwinjilisti Bumijael Mshana.

Watu walioshuhudia tukia hilowalidai kumuona msichana huyo akiangaika kuificha simu hiyo , aina ya TECNO yenye thamani y ash.50,000 mali ya Mboka Petre (26) mkazi wa eneo la Kaloleni mjini hapa.

Akizungumzia hali hiyo Mboka alisema mtuhumiwa huyo alikuwa amekaa kiti kimoja na alianza kufnya zoezi la kumzoea kwa kumbeba motto wake Daniel Jafert (miezi mitano) hatua ambayo ilimfanya kutokuwa na wasiwasi naye hivyo alijikuta ameweka peupe simu yake..

Alisema baada ya kugundua kuwa simu yake haipo alipoiweka alimnongoneza muhudu mmoja wa kanisani hapo ambaye alitoa taarifa kwa mchungaji.

“Mchungaji alichukua uamuzi wa kutangaza kuibiwa kwa simu hiyo kisha alisimamisha shughuli za kutoa sadaka na kuwaomba wote waliokuwa katika foreni wasimame walipo.

Mchungaji Msokwa akizungumzia tukio hilo katika ibada hiyo alisema alipopata taarifa ya wizi huo alisitisha zoezi la kutoa sadaka lililokuwa likiendelea kanisani hapo na kiwataka waumini waliokaa katika kiti hicho akiwemo mtuhuniwa huyo wasimame.

Hatua hiyo ilimpa fursa mchungaji huyo kuanza kuwaita kundi la maombezi pamoja na aliyeibiwa simu kufika madhabauni tayari kwa ajili ya kuombea tukio hilo,kwa imani ya kupata jibu kutoka kwa Mungu..

Suhuda Diana Mlimakithi (15) alisema wakati hali hiyo ikiendelea, alimuona mtuhumiwa akihangaika kuficha simu hiyo kupitia kitenge cha kumbea mtoto huyo aliye achiiwa mtuhumiwa huyo , baada ya mama yake kuitwa na mchungaji kwa lengo la kutoa maelezo mbele ya waumini.

Kitendo hicho kilitoa mwanya wa mtuhumiwa huyo kuangusha simu aliyokuwa ameificha katikatiti lake la kushoto wakati akishuhudiwa na badhi ya waumini wengine akidondosha simu hiyo kwa ujanja.

Baada ya tendo hilo waumini walisemsimu hiyo imepatikana baada ya Tumaini kuidondosha hatua iliyompa nafasi mchungaji kuwaita wazee wa kanisa na kufanya mashauriano katika ofisi yake.

Akizungumza na gazeti hili Tumaini alikiri kuiba simu hiyo ushuhuda ambao aliutoa pia mbele ya waumini wa kanisa hilo huku akiomba msama kuwa tendo hilo hajawahi kulifanya tangu kuzaliwa kwake.

Baada ya tukio hilo Timu ya waombaji walimuombe msichana huyo ambaye wakati wa maombi hayo alidondoka na damu ilianza kumtoka katika baadhi ya maeneo ya mwili wake.

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAJIPANGA KUKABILIANA NA HALI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI.

Kamanga na Matukio | 02:18 | 0 comments
Hawa Mathias,Mbeya.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imejipanga na kuweka mikakati  kushirikiana na wadau mbalimbali  ili kukabiliana na hali ya usafi wa mazingira  nchini na kuhakikisha jamii inatumia vyoo safi na salama  na kuondokana na adha ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi msaidizi,afisa afya mkuu Tanzania  wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Elias Chinamo katika maadhimisho ya siku ya choo duniani yaliyofanyika  wilayani rungwe Mkoani Mbeya.


Alisema kuwa ili kufikia malengo ya mileniam ya utunzaji wa usafi wa mazingira jamii inatakiwa kuwa na mwamko wa kujikita katika kutunza hali ya mazingira  na kujenga vyoo bora ili kuondokana na adha ya kusambaa kwa vinyesi  vinavyochangia  kusababisha magonjwa ya milipuko na kuhara.


Aidha alisema kuwa  katika kufanikisha maadhimisho hayo na tumeweka mikakati ya  kufikisha  ujumbe kwa wananchi   kwa kutoa elimu ya usafi wazingira na matumizi ya vyoo bora  kupitia vipeperushi ,na vyombo vya habari.


"Pia tumeandaa mashindano ya usafi wa mazingira  katika shule za msingi na sekondari ,kata na kaya,na taasisi mbalimbali binafsi na serikalini"Alisema.

Chinamo alifafanua kuwa hali ya usasi wa mazingira ya vyoo bora bado  ni changamoto kubwa nchini na kwamba jitihada za pekee za hitajika  kwani takwimu zinaonyesha   asilimia 12 pekee ya kaya nchini ndizo zenye vyoo bora na salama kwa afya za watumiaji.

WAWILI WAKUTWA NA SILAHA AKIWEMO MWANAMKE- MBARALI.

Kamanga na Matukio | 02:17 | 0 comments
 Hawa Mathias,Mbeya.
Jeshi la polisi Mkoani Mbeya linawashikiliwa watu wawili akiwemo mwanamke  wakazi wa kijiji cha Madibila  na Mkunywa Wilayani mbarali kwa tuhuma za kupatika na silaha pamoja na nyara za serikali  kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  na  kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Athuman Diwani alisema kuwa watuhumiwa hao walikamtwa kwa nyakati tofauti  na askari wa wanayamapori (TANAPA) na akari wa jeshi la polisi walipokuwa katika doria za kusaka waharifu

Alisema kuwa katika tukio la kwanza  Christian Mhangole (40) mkulima alikamatwa na polisi akiwa na  siraha aina ya SMG   yenye namba 88560 ikiwa na risasi 50 ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko maarufu kama( sulphet  ).


Diwani alisema kuwa mara baada ya uchunguzi zaidi mtuhumiwa huyo alibainika kuwa na nyara za serikali ikiwa ni pamoja na nyama ya nyati kilo 15 ,nyama ya tembo kili 17 ambazo zilikuwa zimefichwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kwamba siraha aliyokamatwa nayo imekuwa ikimilikiwa kinyume cha sheria.

Aidha kamanda Diwani alisema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kujihusisha na biashara ya uwindaji haramu wa wanyama pori na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamiliki kujibu tuhuma zinazomkabili.

Katika tukio la pili mwanamke  kijiji cha Mkunywa  wilayani mbarali  Emaliana Ndemo (30) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kupatikana na siraha aina ya Reffle yenye namba B 58221 ikiwa imefichwa  chumbani ndani ya nyumba yake .

Diwani alifafanua kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na jeshi la polisi na kwamba ilikuwa ikitumiwa na mume wa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina za moses  mlingamolo (30) ambaye alifanikiwa kukimbia na  polisi wanaendelea na msako ili aweze kufikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.


Aidha kamanda wa polisi ametoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wanaomiliki siraha kinyume cha sheria kwani wanachangia uvunjifu wa amani kwa wananchi wasiokuwa na hatia na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.

JWTZ MBEYA WAUA BAADA YA MWENZAO KUPIGWA NA WALIINZI WA MADUKA

Kamanga na Matukio | 02:16 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.
 Watu wawili wanadaiwa wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya kuigwa na watu wanadaiwa kuwa ni askari wa JWTZ.

Akiongea na Mtandao huu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMAN amesema katika vurugu hizo mmtu mmoja ndiye aliyeripotiwa amefariki dunia hadi saa ambaye naye bado hajafahamika mara moja na kuongeza kuwa wengine watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ifisi Mbeya.

hata hivyo habari kutoka eneo la Tukio zinadai kuwa Novembeer 17 majira ya saa tano za usiku ktk eneo la DDC mbalizi walinzi wakiwa kwenye doria zao za maduka walimsimamisha askari mmoja wa JWTZ kisha kuanza kumpiga hali iliyopelekea maumivu makali na kukimbilia kwenye kituo cha polisi Mbalizi kwa ajili ya kutoa taarifa.

Badaa ya kufika ktk kituo hicho alipewa huduma mara moja ambapo askari hao waliondokana kwenda eneo la tukio na kuanza kufanya msako wa watu waliohusika hata hivyo usiku hawakufankiwa kumkamata hata mmoja.

siku inayofuata askari hao walifanikiwa kuwakamata walinzi watano na kuanza uchunguzi mara moja ambapo siku hiyohiyo majira ya saa tano za usiku askari wa JWTZ walivamia eneo hilo na kuanza kutembeza kipigo kwa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo kutokana na vurumai hizo watu wawili waliumia vibaya na wengine kujeruhiwa.

aidha watu hao walipelekwa ktk hospital ya Ifisi ambaopo majira ya saa 5 hiyo hiyo wawili kati ya hao waliokuwa wamepigwa walifariki dunia.

Hata hivyo RPC DIWANI alisema kuwa uchunguzi unaendelea kwa ushirikiano wa Polisi na JWTZ kuwapata waliohusika na tukio hilo la uvunjifu wa sheria.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger