Pages


Home » » Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi.

Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi.

Kamanga na Matukio | 04:05 | 0 comments
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie akimkabidhi pikipiki tatu

Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage

Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio Julius Kaijage akimkabidhi pikipiki mbili na matairi 4 ya gari pamoja na mabati mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro vifaa hivyo vyote vimetoka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa




Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na wadau mbali mbali kwenye hafla fupi ya kupokea misaada toka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa

Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki tatu kusaidia jeshi hilo ili zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa Mbeya


Kamanada wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .













Picha ya pamoja
BAADHI ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa mtandao wa ujambazi kutokana na majambazi wengi  kukamatwa na wengine kuawa.
  
Pongezi hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi hilo kuwauwa watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya kurushiana risasi kati ya Askari na majambazi hayo katika tukio lililotokea katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya.
  
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea  kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio  na kuunga mkono juhudi zao, Wadau mbali mbali  leo  wamejitokeza kulichangia jeshi hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa.
  
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana vikiwemo vifaa mbali mbali.
  
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
  
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano zilinunuliwa ambapo kati ya hizo Tatu zimetolewa na Benki ya Nmb kwa thamani ya Shilingi Milion 5.4, wakati kamati ikinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
  
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=, pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni 3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
  
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.

Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya,
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger