Pages


Home » » KILELE CHA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI CHAFANA MBEYA

KILELE CHA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI CHAFANA MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:09 | 0 comments
TUNAWE MIKONO MARA KWA MARA
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Henock Ngonyani, akikata utepe kuzindua bomba la kunawa mikono bomba hilo limetolewa msaada toka kwa klabu ya Rotary  tawi la Mbeya
Baada ya uzinduzi huo hapa mkurugrnzi huyo akinawa mikono kuashiria siku ya unawaji wa mikono duniani
Raisi wa Klabu hiyo Dk Mbinda alisema wamejenga vituo vitatu katika Hospitali hizo mbili kwa gharama ya Shilingi Milioni Tatu na Laki tano(3,500,000/=)kutokana na michango ya kujitolea ya wanachama wapatao 15.
Makirikiri wa Mbeya wakitumbuiza katika kilele cha kunawa mikono Duniani


 
WANANCHI wameaswa kuwa na tabia ya kunawa mikono kila mara hususani wanapotoka Hospitalini kutibiwa ama kuwatembelea wagonjwa ili kujikinga na magonjwa ya maambukizi.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Henock Ngonyani, alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha Siku  ya Kunawa mikono iliyofanyika katika Hospitaliya Rufaa ya Mbeya.

Dk Ngonyani alisema ni vema mamlaka zinazohusika kutoa elimu kwa jamii ili kuwa na tabia ya kunawa mikono yao kwa maji safi na sabuni mara baada ya kutoka kutibiwa au kuwatembelea wagonjwa mawodini ili kuepuaka magonjwa ya kuambukizwa kama kuhara.

Alisema kama Wizara inajukumu la kuandaa miongozo ya namna ya kutibi na kujikinga na magonjwa ya kuambukizwa kwa watumishi wa Afya ambapo tayari Wizara ilikwisha toa miongozo ya Lugha za Kiingereza na Kiswahili ambayo imeshaanza kutumika.
  
Aliongeza kuwa  zaidi ya Watumishi 10,000 wa Huduma za Afya katika Hospitali za Mikoa Wilaya na Rufaa nchi nzima wamepewa mafunzo namna ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukizwa wakati wakihudumia wagonjwa katika Sehemu zao za kazi.
  
“ Ni matumaini yangu kuwa baada ya kutoa elimu kwa Watumishi wa Afya nao pia wataweza kuifikia jamii moja kwa moja kwa kuwaelimisha namna ya kunawa mikono baada ya kutoka Hospitali” alisema Mkurugenzi huyo.


Aliongeza kuwa Zoezi hilo linakabiliwa na Changamoto nyingi ambapo ailizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na ukosefu wa Vitendea kazi kwa Wahudumu ambapo wao wanatakiwa kujikinga kwanza na magonjwa ya kuambukizwa kabla ya kutoa huduma kwa mgonjwa.


Alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Gloves na Eploni za kuvaa watoa huduma kabla ya kuanza kumuhudumia mgonjwa ili asipate magonjwa ya kuambukizwa ambapo aliongeza kuwa upatikanaji wa Vifaa hivyo umekuwa mgumu kutokana na ufinyu wa Bajeti.

  
Changamoto nyingine alisema ni kushindwa kubadilika kwa tabia za baadhi ya Wahudumu kutoka kufanya kazi kwa mazoea na kwenda kwenye kufuata elimu ya kujikinga na magonjwa ya kuambukizwa kutokana na elimu waliyoipata.


Aliitaja Changamoto nyingine kuwa ni Uangamizaji wa taka ngumu zitokanazo na huduma za afya ili kuepukana kabisa na magonjwa ya kuambukizwa ambapo Hospitali nyingi nchini hazina vifaa hivyo na vilivyopo havina uwezo wa kuteketeza taka hizo.

Kutokana na changamoto hiyo Dk. Ngonyani alitoa Wito kwa wadau wa afya kuzipatia msaada Hospitali Nchini wa Vifaa vya kuteketezea taka ngumu ili kumudu zoezi la kukinga na maambukizi ya magonjwa ya kuambukizwa ili jamii iweze kuwa safi.

Kwa upande wake Mratibu wa Zoezi la Kunawa mikono Mkoa wa Mbeya Felister Heller alisema tangu zoezi la kutoa Elimu lianze kumekuwa na mwitikio mkubwa ambapo tangu Mei Mosi Mwaka huu jumla ya watu zaidi ya 6000 wamenawa mikono baada ya kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
  
Alisema Elimu hiyo ilianza kutolewa Mwaka 2005 kupitia Magari ya Matangazo ya barabarani(PA) na  kupitia kwa wagonjwa moja kwa moja kabla ya kuanza kupatiwa matibabu ambapo huambiwa umuhimu wa kunaw mikono baada ya kutoka Hospitalini.

Heller alisema kutokana na mwitikio huo maambukizi ya magonjwa hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kunawa ambapo wengi walikuwa wakipata magonjwa ya kuhara na kipindupindu baada ya kushikana na wagonjwa kisha kula bila kunawa.

Aidha aliishukuru klabu ya Rotary tawi la Mbeya kupitia kwa Raisi Wake Dk Robert Mbinda kwa msaada walioutoa ambao ni kujenga sehemu za kunawia wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na tawi lake katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.
  
Raisi wa Klabu hiyo Dk Mbinda alisema wamejenga vituo vitatu katika Hospitali hizo mbili kwa gharama ya Shilingi Milioni Tatu na Laki tano(3,500,000/=)kutokana na michango ya kujitolea ya wanachama wapatao 15.

 Picha na Mbeya yetu
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger