MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw.
Chripin Meela amesema, changamoto zinazokabili sekta ya habari na vyombo
vya habari kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma hiyo katika ukuaji
wa demokrasia nchini.
Akizungumza kwenye mkutano wa
uchaguzi wa klabu ya wandishi wa habari mkoa Mbeya Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Chrispin Meela amesema, wananchi wana matumaini makubwa na vyombo vya
habari na pale kipapota doa la utendaji ni muhimu kujirekebisha kabla ya
kutengeza picha mbaya mbele ya jamii wanayoihudumia.
Amesema hali iliyojitokeza hivi
karibuni kwenye klabu hiyo inahitaji kuweka misingi imara ya kiutendaji
na kwamba jitihada za kufanya uchaguzi wakati huu ni hatua muhimu za
kuimarisha mfumo wa kujiwajibisha kama taasisi ya taaluma.
Amesema ikiwa viongozi wa dini na
vyombo vya habari vitajihusisha na ubadhirifu na wizi ni dalili kuwa hakutakuwa
na mwingine wa kukemea jamii itakayokuwa huru na yenye kukemea vita dhidi ya
rushwa.
Bwana Meela amesema inashangaza
kuona hata vyombo vya habari vinaingia kwenye ufisadi na akaohoji ninani
atakayehoji ufisadi serikali na kwingineko kama nanyi mnaingia kwenye mitego
hiyo hiyo?.
Katika hatua nyingine amependekeza
Vyombo vya habari kujenga utamaduni wa kujihusisha na ufuatiliaji wa
maendeleo vijijini na kwa kufanya hivyo kutawezesha wananchi kuwasilisha
changamoto zinazowakabili kwa watunga sera.
Amesema katika kufikia hilo
ni vyema pia Viongozi wa serikali ngazi za chini kuondoa uoga katika
kufanya kazi na vyombo vya habrari na kwa kufanya hivyo kutasadia kusukuma
mbele jitihada za maendeleo.
Katika hatua nyingine Bwana Meela
amechangia kiasi cha shilingi 400,000 kwaajili ya uanzishaji wa chama cha
kuweka na kukopa cha wanahabari SACCOS ili kuwezesha kuwapa fulsa
wana habari kujisimamia kiuchumi na kupunguza changamoto za
kimaisha zinazowakabili.
Katika kufanikisha hilo wanachama
wa Mbeya Press club walijitokeza kuchangishana wenyewe ambapo wamefanikiwa
kukusanya mtaji wa papo kwa papo kiasi cha shilingi 1,400,000/=.
Aidha ameshauri klabu ya wandishi
wa habari kuwa na ofisi yake na hvyo kwa kuomba kiwanja kwenye mamlaka za
majiji itasaidia kuwapa nguvu katika kusimamia haki zao wakiwa na uhuru wa
kuwekeza kwenye majengo yao.
Habari na Indaba Africa
picha na Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment