Pages


Home » » Momba, wamependekeza Mkoa mpya utakaogawanywa na serikali upewe jina la Momba, ukijumuhisha Wilaya ya Momba, Mbozi, Ileje na Chunya huku makao makuu yakiwa Vwawa.

Momba, wamependekeza Mkoa mpya utakaogawanywa na serikali upewe jina la Momba, ukijumuhisha Wilaya ya Momba, Mbozi, Ileje na Chunya huku makao makuu yakiwa Vwawa.

Kamanga na Matukio | 03:57 | 0 comments

 Mkuu wa Wilaya ya Momba, Abiudi Saideya amesema Mkoa wa Mbeya utabaki kama ulivyo huku ukiunganisha Wilaya ya Mbeya, Kyela, Rungwe na Mbarali.
Mkurugenzi Halmashauri ya Momba
Wakitoa mapendekezo yao baadhi ya wajumbe, walisema kuwa Wilaya ya Momba inavivutio vya kiutalii, idadi ya watu, mazao ya chakula na biashara kama vile ufuta, kahawa, mahindi, mpunga  pamoja na uoto wa asili.


Timu ya wataalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Momba, wamependekeza Mkoa mpya utakaogawanywa  na serikali upewe jina la Momba, ukijumuhisha Wilaya ya Momba, Mbozi, Ileje na Chunya huku makao makuu yakiwa Vwawa.
Pendekezo hili wamelitoa jana, kwenye kikao cha Kamati ya ushauri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo eneo la Ukwile Wilayani Mbozi kutokana n kutokamilika kwa baadhi ya miundombinu ya wilaya ya Momba.
Kikao hicho kilichokuwa kikijadili maendeleo ya Wilaya kiliendeshwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Abiudi Saideya na kwamba Mkoa wa Mbeya utabaki kama ulivyo huku ukiunganisha Wilaya ya Mbeya, Kyela, Rungwe na Mbarali.
Aidha, mapendekezo hayo yamekuja ni baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muunganano akiwa Mkoani Mbeya kwenye sherehe za mei mosi kuridhia ombi la serikali kuugawa Mkoa wa Mbeya kutokana na ukubwa wa eneo za mraba zilizopo.
Wakitoa mapendekezo yao baadhi ya wajumbe, walisema kuwa Wilaya ya Momba inavivutio vya kiutalii, idadi ya watu, mazao ya chakula na biashara kama vile ufuta, kahawa, mahindi, mpunga  pamoja na uoto wa asili.
“Momba ndio kitovu cha barabara kuu iendayo nchi za kusini mwa Afrika endapo utapewa hadhi ya Mkoa utaongeza kipato kupitia ushuru wa forodha kwa nchi za kusini mwa afrika,”alisema Saideya
 Pia, kikao hicho kilitumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo vya watu kutokana na vitendo vya kishirikina ambavyo vimetajwa kukithiri katika Wilaya hiyo.
Saideya, aliwataka waganga wa kienyeji ambao wanashughulika na upigaji wa ramli kuacha mara moja kwani wao ndio chanzo cha mauaji hayo.
Alisema, waganga wanapopiga ramli huwataja baadhi ya watu kwamba ndio wamesababisha kifo cha mgonjwa Fulani hivyo kupelekea watu kutengeneza uadui hadi kufika mahala wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuondoa uhai wa watu hao wanaotajwa na waganga.

“Hivi karibuni katika kijiji cha Msangano, watu watatu walizikwa wakiwa hai kutokana na ramli hizi za waganga jambo linalotia dosari Wilaya ikiwa na kudumaza maendeleo kwani watu wanaogopa kuwekeza biashara zao,”alisema
Hata hivyo, Mkuu huyo aliwataka wakazi wa eneo hilo kujenga tabia ya kutunza chakula hasa kwenye msimu huu wa mavuno kwani kumekuwepo na dalili za nje kutokana na hali ya ukame inayoendelea Wilayani humo.

Picha na Ezekiel Kamanga
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger