Home »
» WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUWAWA NA POLISI MKOANI MBEYA
WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUWAWA NA POLISI MKOANI MBEYA
|
Baadhi ya wananchi wakitoka kutambua miili ya wanaodhaniwa kuwa ni majambazi |
|
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi kwani mpaka sasa maiti hizi hazijatambulika |
|
Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika siraha |
|
Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo |
|
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo |
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa
Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana
katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya
Tukuyu.
|
|
Kamanda Diwani akikagua gari ya majambazi yaliouwawa
MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya
umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni
majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani
amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo
majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika
Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za
Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao
wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota
Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea
Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza
kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa
kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa
wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi
walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye
magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba
94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za
Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika
maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini
Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao
hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa
zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe
kazi.
Picha na Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment