Home »
» SHIRIKA LA POSTA LAONYESHA UHAI WAO
SHIRIKA LA POSTA LAONYESHA UHAI WAO
|
LEONARD YEGELLA MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA AKIPOKEA ZAWADI YA MFANYAKAZI BORA TOKA KWA RAISI |
|
MKOSA
SHABANI MADANGANYA AKIPOKEA ZAWADI KUTOKA KWA MWAKILISHI WA MKURUGENZI
WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KATIKA HAFLA ILIYOFANYKA KATIKA UKUMBI WA
MKAPA JIJINI MBEYA |
|
GENOVEVA ASSENGA KARANI WA SHIRIKA LA POSTA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM NAYE AKIPOKEA TUZO YA MFANYAKAZI BORA |
|
YEGELLA AKIPONGEZWA NA VIONGOZI WAKE |
|
MAGRETH MABULA AKIPEWA ZAWADI YA MFANYAKAZI BORA KUTOKA SHIRIKA LA POSTA MKOA WA MBEYA |
|
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA WAKISHANGILIA KWA FURAHA |
|
AFISA
UHUSIANO WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA BWANA MIIGO AKIZUNGUMZA JAMBO
WAKATI WA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA SHIRIKA HILO |
|
MENEJA
WA SHIRIKA LA POSTA MKOA WA MBEYA HASSAN MWANG'OMBE AKIZUNGUMZA NA
WAFANYAKAZI (HAWAPO PICHANI) KATIKA HAFLA YA KUWAPONGEZA WAFANYAKAZI
WAO.
WATUMISHI wa Umma na sekta binafsi nchini
wameaswa kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi katika
kuziletea manufaa sekta wanazofanyia kazi.
Mwito huo umetolewa na baadhi ya Wafanyakazi wa
Shirika la Posta Tanzania ambao wametunukiwa Zawadi za wafanyakazi
bora kutokana na utendaji kazi wao baada ya kupigiwa kura na watumishi
wenzao.
Wakizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa
na uongozi kwa wafanyakazi wote iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa
uliopo Sokomatola Jijini Mbeya baada ya kupewa nafasi ya kuwashukuru wenzao kwa
kuwawezesha kuchaguliwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
Leonard Yegella (Principal Finance
Officer- usimamizi)ambaye pia alitunukiwa zawadi ya mfanyakazi bora na Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alisema anafurahia
kupewa nafasi kama hiyo ambayo ameipata kutokana na ushirikiano mzuri na
wafanya kazi wenzie.
Wengine waliotunukiwa zawadi na Uongozi wa Posta
ni pamoja na Bi Genoveva G. Assenga karani wa Posta kutoka makao makuu Dar Es
Salaam, Bi Magreth Mabula na Mkosa Shaban Madanganya walioibuka wafanyakazi
bora kutoka Mkoa wa Mbeya.
Picha na Ezekiel Kamanga & Mbeya Yetu Blog.
|
0 comments:
Post a Comment